settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya kupitia Dolorosa?

Jibu


Njia ya Dolorosa, kwa halisi ni "njia ya huzuni," ni njia ya jadi huko Yerusalemu ambayo Bwana wetu alisafiri siku ya kusulubiwa kwake kutoka kiti cha hukumu cha Pilato, pia aitwaye Mtawala (Mathayo 27: 2-26), hadi mahali pa kusulubiwa kwake juu ya Mlima Kalvari. Baada ya hukumu yake na Pontio Pilato, Bwana Yesu alipigwa, alidhiakiwa na kutemewa mate na askari wa Kirumi (Mathayo 27: 26-31). Kisha alilazimika kuubeba msalaba Wake mwenyewe kupitia barabara za Yerusalemu hadi Golgotha, ambako alisulubiwa (Mathayo 27: 32-50). Kwa sasa njia ya Dolorosa ina alama ya vituo "kumi na nne vya msalaba" kukumbuka matukio kumi na manne ambayo yanadhaniwa kufanyika njiani. Bila shaka matukio haya tano hayajaandikwa katika Biblia, badala yake yanachibuka toka mila ya Katoliki. Kati ya hizo zilizotajwa katika Maandiko, mahali halisi pa matukio njiani, kama vile mhali pa kupigwa mijeledi (Yohana 19: 1-3) na kubebewa msalaba na Simoni Mkirene (Mathayo 27:32), hayajulikani.

Biblia haitaji hasa moja kwa moja njia ya Dolorosa. Yote tunayoyajua kutoka kwa Maandiko ni kwamba Yesu alichukua msalaba Wake kutoka kwa Makao ya gavana Waroma hadi kwenye kwenye Mlima Kalvari ambapo alisulubiwa. Eneo la maeneo haya mawili haijulikani kwa uhakika, lakini popote walipokuwa, njia waliyoipitia ilikuwa ya huzuni sana. Mateso na maumivu ya kimwili ambayo Bwana Yesu aliteseka yalikuwa kidogo ikilinganishwa na maumivu yaliyosababishwa na mzigo halisi uliosababisha aliyoyapitia — mzigo wa dhambi za waumini wote. Alibeba dhambi zetu msalabani ambapo alilipa adhabu kwa wote.

Wakristo wanapotafakari safari ya Kristo msalabani, tunakumbushwa nini zawadi ya thamani ya wokovu wetu na bei iliyolipwa na Bwana Yesu. "Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona" (Isaya 53: 5). Tunapofikiria juu ya maumivu na udhalilisho Yeye aliteseka kwa ajili yetu, kulipa bei ambayo hatuwezi kulipa wenyewe, hatuwezi kujisaidia lakini kumsifu na kumshukuru na kuyatoa maisha kwa kumtii.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya kupitia Dolorosa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries