settings icon
share icon
Swali

Desturi ya kupiga kura ni nini?

Jibu


Desturi ya kupiga kura imetajwa mara sabini katika Agano la Kale na mara saba katika Agano Jipya. Licha ya marejeleo mengi ya kupiga kura katika Agano la Kale, hakuna kitu kinachojulikana kuhusu kura halisi. Labda ilikuwa fimbo ya urefu mbalimbali, mawe yaliyo nyooka kama sarafu, au aina fulani ya kete; lakini asili yao halisi haijulikani. Desturi ya kisasa ambayo ni sawia na kupiga kura ni kugeuza sarafu.

Desturi ya kupiga kura hutokea mara nyingi zaidi kuhusiana na mgawanyiko wa ardhi chini ya Yoshua (Yoshua sura ya 14-21), utaratibu ambao Mungu aliwaagiza Waisraeli mara kadhaa katika kitabu cha Hesabu 26:55, 33:54 ; 34:13; 36: 2). Mungu aliruhusu Waisraeli kupiga kura ili kuamua mapenzi Yake kwa hali fulani (Yoshua 18: 6-10, 1 Mambo ya Nyakati 24: 5,31). Ofisi mbalimbali na kazi katika hekaluni pia ziliamuliwa kwa kura (1 Mambo ya Nyakati 24: 5, 31; 25: 8-9; 26: 13-14). Wasafiri wa meli ya Yona pia walipiga kura ili kuamua nani aliyeleta ghadhabu ya Mungu juu ya meli yao (Yona 1: 7). Mitume kumi na mmoja walipiga kura ili kuamua nani atakayechukua nafasi ya Yuda (Matendo 1:26). Kutupa kura hatimaye ikawa ni mchezo watu walicheza na kubahatisha. Hii inaonekana katika askari wa Kirumi wakipiga kura kwa mavazi ya Yesu (Mathayo 27:35).

Hakuna mahali katika Agano Jipya ambapo Wakristo wanaagizwa kutumia njia inayofanana na kupiga kura ili kusaidia kufanya maamuzi. Sasa kwa kuwa tuna Neno la Mungu lililokamilishwa, pamoja na Roho Mtakatifu anayeishi ndani yate na kutuongoza, hakuna sababu ya kutumia michezo ya nasibu ya kufanya maamuzi. Neno, Roho, na sala ni vya kutosha katika kutambua mapenzi ya Mungu leo-si kupiga kura, kupiga kete, au kugeuza sarafu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Desturi ya kupiga kura ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries