settings icon
share icon
Swali

Kwa nini kuwapenda wengine mara nyingi ni vigumu sana?

Jibu


Kuwapenda wengine inaweza kuwa ngumu sana wakati mwingine. Maneno ya kawaida ya kutaja watu hao ambao sisi daima hukujikuta katika hali ngumu ya kupenda ni watu "neema zaidi inahitajika". Lakini hata watu ambao tunawapenda kwa wakati mwingine huwa vigumu kuwampenda. Sababu kuu tunayo shida katika kuwapenda wengine ni dhambi, zote zetu na za wale tunajaribu kuwapenda. Binadamu ni viumbe vilivyoanguka. Mbali na Mungu na nguvu zake, sisi ni wabinafsi, na kujipenda wenyewe huja kwa kawaida zaidi kuliko kupenda wengine. Lakini upendo hauna ubinafsi; inatafuta yaliyo bora kwa wengine (1 Wakorintho 13: 5; Wafilipi 2: 3). Kupigana na ubinafsi wetu wenyewe na tamaa za dhambi na kushughulika na ubinafsi na tamaa za dhambi za wengine zinaweza kufanya upendo uwe kazi.

Sababu nyingine inaweza kuwa ni vigumu kwetu kuwapenda wengine ni kwamba wakati mwingine hatujui ni nini upendo wa kweli. Tunapenda kufikiria upendo kama majibu ya kihisia. Tatizo ni kwamba hatuwezi kudhibiti kila hisia zetu. Kwa hakika tunaweza kudhibiti kile sisi hufanya kwa sababu ya hisia, lakini mara nyingi hisia zenyewe hutokea. Lakini aina ya upendo Mungu anatuita kuwa nao kwa wengine ni aina ile ile aliyo nayo kwa ajili yetu. Ni upendo wa dati (agape), kiini chake ni dhabihu. Upendo wa Mungu kwetu ni upendo wa dhabihu, aina ambayo imemtuma msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye hakutuokoa kwa sababu tulimpenda; Alituokoa kwa sababu upendo wake ulimfanya Ajitoe nafsi yake kwa ajili yetu. Je, tunawapenda wengine ya kutosha kuwalipia dhabihu, hata wakati hawapendeki? Kuwapenda wengine ni suala la mapenzi, sio hisia.

Mungu alikufa kwa ajili yetu katika hali yetu mbaya zaidi, katikati ya dhambi zetu, wakati tulikuwa hatupendeki kabisa (Warumi 5: 8; Yohana 15:13). Tunapojitoa dhabihu ili kumpenda mtu, tunapata maelezo ya kina cha upendo wa Mungu kwa ajili yetu, na pia tunamwonyesha kwa ulimwengu. Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi"(Yohana 13: 34-35). Ana Yeye hakusema, "jihisi kupendana." Alisema, "Mpendane." Aliamuru hatua, sio hisia.

Sehemu ya ugumu wa kupenda wengine ni kwamba mara nyingi tunataka kujaribu kufanya hivyo sisi wenyewe, kukusanya hisia za upendo ambapo hakuwepo hata moja. Hii inaweza kusababisha uongo na "mchezo wa kuiga" sehemu ya mtu mwenye upendo, wakati mioyo yetu ikiwa hati hati kuhusu wengine. Lazima tuelewe kwamba hatuwezi kupenda mbali na Mungu. Wakati tunapokaa katika Yesu (Yohana 15) na Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu kwamba tunaweza kuzaa matunda ya upendo (Wagalatia 5: 22-23). Tunaambiwa kwamba Mungu ni upendo na kwamba upendo wetu kwa wengine unawezeshwa na Mungu na itikio kwa upendo wake ndani yetu (1 Yohana 4: 7-12). Inaweza kuwa vigumu kwetu kutegemea Mungu na kujitoa kwake, lakini pia anaruhusu ugumu huu ili utukufu Wake uweze kuonekana zaidi. Tunapopenda watu ambao ni wagumu au kuchagua kupenda hata wakati hatujisiki, tunadhihirisha kumtegemea Mungu na kuruhusu nguvu Yake kuonyeshwa kupitia kwetu.

Kuwapenda wengine ni ngumu kwa sababu wao ni wanadamu na sisi ni wanadamu. Lakini katika ugumu huu tunakuja kufahamu vizuri ubora wa upendo wa Mungu kwetu. Na tunapowapenda wengine licha ya ukosefu wao wa kutosha, Roho wa Mungu huangaza, Yeye hutukuzwa, wengine hujengwa, na ulimwengu unaona Kristo ndani yetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini kuwapenda wengine mara nyingi ni vigumu sana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries