settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu Wakristo kutumia njia ya upangaji uzazi?

Jibu


Mwanadamu alipewa jukumu na Mungu “Zaeni mkaongezeke” (Mwanzo 1:28). Ndoa ilianzishwa na Mungu kama masingara thabiti ambayo kwayo tutazaa na kuwalea watoto. Cha kushangaza, watoto siku hizi wakati mwingine wanachukuliwa kama vitu bure na mzigo. Wako tu katikati ya taaluma ya watu na malengo yao ya kifedha na “wanatia mawimbi katika mitindo yetu” ya ujamii. Kila mara aina hii ya uchoyo mizizi yako iko katika utumiaji wa tepembe za upangaji uzazi.

Kinyume na kujipenda kando mwa njia za upangaji uzazi mwingi, Bibilia inawadhihirisha watoto kama zawadi kutoka kwa Mungu (Mwanzo 4:1; Mwanzo 33:5). Watoto ni urithi kutoka kwa Bwana (Zaburi 127:3-5). Watoto ni Baraka kutoka kwa Mungu (Luka 1:421). Wana wa wana ndio taji kwa wazee (Methali 17:6). Mungu anambariki mwanamke tasa na watoto (Zaburi 113:9; Mwanzo 21:1-3; 25:21-22; 30: 1-2; 1 Samweli 1:6-8; Luka 1:7, 24-25). Mungu anawatengeneza watoto katika tumbo (Zaburi 139:13-16). Mungu anawajua watoto kabla wazaliwe (Yeremia 1:5; Wagalatia 1:15).

Vile Bibilia inavyo kujakaribia kwa kushutumu upangaji uzazi katika Mwanzo mlango wa 38, hesabu ya wana wa Eri na Onani. Eri alimwoa mwanamke aitwaye Tamari, lakini alikuwa mwenye dhambi na Bwana akamwua, na kumwacha Tamari bila mume au watoto. Tamari aliozwa kwa nduguye Eri, Onani, kulingana na sheria ya ndoa ya ukoo katika Kumbukumbu la Torati 25:5-6. Onani hakutaka kugagwanyisha urithi wake kwa mtoto yeyote ambaye angemzalia nduguye, kwa hivyo akatumia mtindo wa zamani wa upangaji uzazi, wa kutoa nje. Mwanzo 38:10 yasema, “Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye naye.” Onani nia yake ilikuwa ya kibinafsi/uchoyo: alimtumia Tamari kwa manufaa yake mwenyewe, lakini akakataa kutekeleza jukumu lake kisheria la kumzaa mrithi wa marehemu nduguye. Ufahamu huu kila mara watumika kama thibitisho kuwa Mungu haitikii upangaji uzazi. Ingawa, haikuwa kabisa tendo la kutumia tembe za upangaji uzazi ambazo zilimfanya Mungu amwue Onani; bali ilikuwa tama iliyokuwa katika kitendo.

Ni vyema kuwaona watoto vile Mungu anavyowaona, sio vile ulimwengu unatuambia tunavyostahili kuwaona. Nikisha sema hayo, Bibilia haikani tembe za kupanga uzazi. Tembe za kupanga uzazi ni kinyume na kupata mimba. Sio tendo la tembe litakalo bainisha kama ni vibaya au ni vyema. Vile tulijifunza kutoka kwa Onani, ni msukumo ulio nyuma ya tendo la vizuizi ambao unaamua kama uko sawa au uko na ubaya . kama wanandoa wanatumia vizuizi vya mimba ili wapate muda mwingi kwa wao wenyewe, basi hiyo ni mbaya. Ikiwa wanandoa watumia vizuia mimba ili kwa muda wakawishe kupata mtoto hadi pale wamekomaa na wamejitayarisha kifedha na kiroho, basi hiyo imekubalika kutumia vizuia mimba kwa muda. Tena yote iturudi kwa msukumo.

Bibilia kila mara yaliweka swala la kupata watoto kuwa jambo jema. Bibilia “yatarajia” kwamba mume na mke wawe na watoto. Kutokuwa na uwezo wa kupata watoto umewazilizwa katika Bibilia kuwa jambo baya. Hakuna mtu katika Bibilia anayeonyesha nia ya kutopata watoto. Kwa wakati huo, haiwezi jadiliwa kutoka kwa Bibilia kuwa ni makosa kutumia njia za kupanga uzazi kwa muda mfupi. Wanandoa wote ambao wameolewa lazima watafute mapenzi ya Mungu hasa kuambatana na ni lini wanastahili kuwa na watoto na ni watoto wangapi wanataka kupata.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu Wakristo kutumia njia ya upangaji uzazi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries