settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kuosha miguu?

Jibu


Katika nyakati za Biblia, hali ya vumbi na uchafu ya mkoa na kuvaa viatu kulihitaji kuosha miguu. Ijapokuwa wanafunzi wengi wangefirajo kuosha miguu ya Yesu, lakini hawakuweza kuichukulia kiurahisi dhana kuoshana miguu. Hii ilikuwa kwa sababu katika jamii ya wakati huo, kuoshwa kwa miguu ilihifadhiwa kwa watumishi wa chini kabisa. Wenzi hawakuosha miguu, isipokuwa mara chache sana na kama alama ya upendo mkubwa. Luka anasema kwamba wanafunzi walikuwa wakilalamika juu ya nani aliye mkuu zaidi kati yao (Luka 22:24), mtazamo unaozuilia nia ya kushwa kwa miguu. Yesu alipokusongea ili kuwaosha miguu, walishtuka (tazama pia Yohana 13: 1-16). Matendo yake hutumika pia kama mfano wa utakaso wa kiroho (Yohana 13: 6-9) na mfano wa unyenyekevu wa Kikristo (Yohana 13: 12-17). Kwa kuosha miguu ya wanafunzi wake, Yesu alifundisha somo la huduma isiyo ya ubinafsi ambayo ilikuwa mfano mkubwa kwa kifo chake msalabani.

Kuoshwa kwa miguu ilikuwa mfano, mtindo. Vikundi vingi katika historia ya kanisa wamefanya mazoezi ya kusha miguu halisi ya kama sheria ya kanisa. Hata hivyo, utamaduni wa sasa katika nchi nyingi hauitaji kuosha vumbi kutoka kwa miguu ya wageni wa mtu. Ingawa Mlo wa Bwana ulifanyika, kanisa la kwanza halikufanya kuosha miguu kama amri katika mikusanyiko ya kanisa.

Yesu kuosha miguu ya wanafunzi wake inasisitiza unyenyekevu wa ndani, sio ibada ya kimwili. Tendo laule mjane Mkristo la "kuosha miguu ya watakatifu" (1 Timotheo 5:10) halizungumzii kuhusika kwake katika maagizo ya kanisa bali kwa huduma yake ya unyenyekevu, kama mtumwa kwa waumini wengine. Kukataa kufuata mfano wa Yesu ni kujiinua juu kibinafsi na kuishi kwa kiburi. "Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake" (Yohana 13:16).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kuosha miguu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries