settings icon
share icon
Swali

Je! Wakristo wanapaswa kuomba msamaha kila wakati kwa dhambi zao?

Jibu


Swali la mara kwa mara ni "Ni nini kinachotokea kwa dhambi, ikiwa mimi nitafa kabla ya kuwa na nafasi ya kukiri dhambi kwa Mungu?" Swali lingine la kawaida ni "Ni nini kinachotokea kama mimi nimetenda dhambi, lakini kisha nisahau kuikiri hiyo dhambi kwa Mungu?" Maswali haya yote msingi wake uu katika dhana mbaya. Wokovu si jambo la waumini kujaribu kukiri na kutubu kila dhambi wao wamefanya kabla ya kufa. Wokovu msingi hauko kama Mkristo amekiri na kutubu kila aina ya dhambi. Naam, tunapaswa kukiri dhambi zetu kwa Mungu pindi tu tunapofahamu kwamba tuna dhambi. Ingawaje sio kila mara twastahili kumuomba Mungu msamaha. Tukiweka imani yetu katika Yesu Kristo kwa ajili ya wokovu, dhambi zetu zote zimesamehewa. Hiyo ni pamoja na dhambi za siku za nyuma, sasa na za baadaye, kubwa au ndogo. Waumini hawapaswi kuomba msamaha au kutubu kila wakati ili wasamehewe dhambi zao. Yesu alikufa ili alipe adhabu kwa ajili ya dhambi zetu zote, na wakati zimesamehewa, zote zimesamehewa (Wakolosai 1:14, Matendo 10:43).

Chenye sisi tunafaa kufanya ni kukiri dhambi zetu: "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote" (1 Yohana 1:9). Kile mstari huu unatuambia tufanye ni "kuungama" dhambi zetu kwa Mungu. Neno "kukiri" maana yake "kukubaliana na." Wakati tunaziungama dhambi zetu kwa Mungu, sisi hukubaliana na Mungu kuwa tuko na makosa, kwamba tuna dhambi. Mungu hutusamehe tunapokiri, kwa hali inayoendelea kwa sababu ya ukweli kwamba Yeye ni "mwaminifu na wa haki." Ni kwa jinsi gani Mungu ni mwaminifu na wa haki?" Yeye ni mwaminifu kwa kusamehe dhambi, ambayo ameahidi kufanya kwa ajili ya wanaompokea Kristo kama Mwokozi wao. Yeye hutumia malipo ya Kristo kwa ajili ya dhambi zetu, na kutambua kuwa dhambi zao kweli zimepata kuoshwa .

Wakati huo huo, 1 Yohana 1:9 inaonyesha kwamba kwa namna fulani msamaha hutegemea vile tunapokiri dhambi zetu kwa Mungu. Jinsi gani hii inafanya kazi kama dhambi zetu zote zimesamehewa wakati tumempokea Kristo kama Mwokozi? Inaonekana kwamba kile mtume Yohana anakielezea hapa ni "uhusiano" wa msamaha. Dhambi zetu zote zimesamehewa "hasa "wakati sisi humpokea Kristo kama Mwokozi. Huu msamaha halisi ndio unaotuhakikishia wokovu wetu na ahadi ya uzima wa milele mbinguni. Wakati sisi tunasimama mbele ya Mungu baada ya kifo, Mungu hawezi kutukatasa kuingia mbinguni kwa sababu ya dhambi zetu. Huo ndio msamaha wa halisi. Suala la msamaha wa uhusiano ni, huzingatia ukweli kwamba wakati sisi hutenda dhambi, sisi humkosea Mungu na kumhuzunisha yule Roho wake (Waefeso 4:30). Huku kukiwa kwamba Mungu ametusamehe dhambi ambazo tumetenda, bado husababisha kizuizi katika uhusiano wetu na Mungu. Mtoto ambaye ametenda dhambi dhidi ya baba yake hatupwi nje ya familia. Baba mcha Mungu atawasamehe watoto wake bila masharti. Wakati huo huo, uhusiano mzuri kati ya baba na mwana hauwezi kupatikana mpaka uhusiano hurejeshwe. Hii inaweza tu kutokea wakati mtoto anakiri makosa yake kwa baba yake na kuomba msamaha. Hiyo ndio sababu kwa nini tunaziungama dhambi zetu kwa Mungu, si kwa kudumisha wokovu wetu, bali tunajileta wenyewe katika ushirika wa karibu na Mungu ambaye anatupenda na tayari amekwisha tusamehe dhambi zetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Wakristo wanapaswa kuomba msamaha kila wakati kwa dhambi zao?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries