settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inakuza au kuzuia kuomba kwa malaika?

Jibu


Ingawa hakuna aya ambayo inasema waziwazi, "Usiombe kupitia malaika," ni dhahiri sana kwamba hatupaswi kuomba kwa malaika. Hatimaye, sala ni tendo la ibada. Na, kama vile malaika wanakataa ibada yetu (Ufunuo 22: 8-9), kwa hiyo watakataa pia maombi yetu. Kutoa ibada yetu au sala kwa mtu yeyote isipokua Mungu ni ibada ya sanamu.

Pia kuna sababu kadhaa za kitendo na za kitheolojia kwa nini kuomba kwa malaika kuna makosa. Kristo mwenyewe hakuwahi kumwomba yeyote bali Baba. Alipoulizwa na wanafunzi wake kuwafundisha jinzi ya kuomba, aliwaagiza "Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba: Baba yetu wa mbinguni ..." (Mathayo 6: 9; Luka 11: 2). Ikiwa kuomba kwa malaika ni kitu ambacho sisi, kama wanafunzi wake, tunapaswa kufanya, hii ingekuwa mahali pa Yeye kutuambia. Kwa wazi, tunapaswa kuomba tu kwa Mungu. Hii pia inaonekana katika Mathayo 11: 25-26, ambapo maombi ya Kristo huanza, "Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbinguni na nchi ...." Yesu aanzi sala zake kwa kumwambia Baba, lakini yaliyomo ndai ya Sala yake mara nyingi huomba msaada ambao unaweza tu kupewa na mtu mwenye nguvu, mwenye ufahamu, na mamlaka yoyote. Kuomba kwa malaika hakutakuwa na ufanisi kwa sababu ni viumbe na hawana mamlaka haya.

Yesu anaomba kwa niaba ya wafuasi wake katika Yohana 17: 1-26, akiwaombea baraka nyingi kutoka kwa Mungu Baba, ikiwa ni pamoja na utakaso, utukufu, na kuhifadhiwa. Baraka hizi tatu zinaweza tu kuja kutoka chanzo ambacho sasa kinashishikilia. Tena, malaika hawana nguvu hii. Malaika hawezi kututakasa, hawezi kututukuza, na hawezi kutuhakikishia urithi wetu katika Kristo (Waefeso 1: 13-14).

Pili, kuna tukio katika Yohana 14:13 wakati Kristo mwenyewe anawaambia waumini kuwa chochote tunachoomba kwa jina lake, Yeye atatimiza kwa sababu anaomba moja kwa moja kwa Baba. Kutoa sala kwa malaika kutapungukiwa na maombi yenye ufanisi yanayoongozwa na Biblia (ona pia Yohana 16:26). Hakuna Malaika wala kitu chochote kile ambacho kimetengenezwa kuwa ni msaidizi na Baba yetu. Mwana tu na Roho Mtakatifu (Warumi 8:26) anaweza kutuombea mbele za kiti cha Baba.

Mwisho, 1 Wathesalonike 5:17 inamwaambia mwamini kuomba bila kukoma. Hii itawezekana pekee ikiwa muumini anaweza kumfikia Mungu ambaye daima youpo na anapatikana ili ayazikilize maombi ya kila mtu wakati huo huo. Malaika hawana uwezo huu-hawana uwezo wa kuwa kila mahali au kuwa wenye nguvu-na hawana sifa ya kupokea sala zetu. Maombi kwa Baba kupitia Kristo ndio njia pekee muhimu na yenye ufanisi ambayo tunaweza kuwasiliana na Mungu. La hasha, kuomba kwa malaika sio dhana ya kibiblia kabisa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inakuza au kuzuia kuomba kwa malaika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries