settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuomba katika jina la Yesu?

Jibu


Maombi katika Jina la Yesu linafunzwa katika Yohana 14:13-14, “Ninyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ila Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu nitalifanya.” Wengine wanaitumia vipaya aya hii, wakidhani kwamba kwa kusema “kwa jina la Yesu” katika mwisho wa maombi yao, huwa Mungu ajibu mahitaji yao. Hii hasa nikuchukulia maneno, “katika jina la yesu” kuwa utaratibu wa kiuchawi. Hii kamwe ni kinyume na Bibilia.

Kuomba katika jina la Yesu, yamaanisha kuomba kwa mamlaka yake na kumwomba Mungu Baba kutendea maombi yetu kwa sababu tunakuja kwa jina la Mwanawe, Yesu. Kuomba katika jina la Yesu yamaanisha kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu, “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14-15). Kuomba katika jina la Yesu ni kuomba vitu ambavyo vinamweheshimu na kumtukuza Yesu.

Kusema, “katika jina la Yesu” mwisho wa maombi sio utaratibu wa kiuchawi. Kama chenye tunauliza, au kusema katika maombi sio utukufu wa Mungu na kulingana na mapenzi yake, kusema, “katika jina la Yesu” haina maana. Kuomba kwa ukweli katika jina la Yesu na kwa utukufu wake ndio jambo la maana, sio kuambatanisha maneno mengine mwisho wa maombi. Sio maneno katika maombi ambayo yana umuimu, ni lengo ambalo liko nyuma ya maombi. Kuomba mambo ambayo yanaambatana na mapenzi ya Mungu ndio asili ya kuomba katika jina la Yesu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuomba katika jina la Yesu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries