settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kuoa tena baada ya kifo cha mwenzi wako?

Jibu


Je! Mtu anaweza kuoa tena baada ya yeye kuwa mjane? Biblia haijasema kuwa ni makosa kuoa tena baada ya mwenziwe kufa, katika matukio mengine hata inaihimiza kuoa tena(1 Wakorintho 7: 8-9; 1 Timotheo 5:14). Utamaduni wa Kiyahudi katika nyakati za Biblia pia ulihimiza hili kwa sababu tofauti. Katika hali nyingi, Biblia inazungumzia suala la wajane badala ya wajane wa kiume. Hata hivyo, hakuna kitu ndani ya vifungu hivi vinavyotuwezesha kuamini kwamba ilikuwa juu ya jinsia maalum.

Kimsingi kuguzia suala la wajane kunawezekana kuwa kwa sababu tatu. Ya kwanza ni kwamba wanaume walifanya kazi nje ya nyumba, wakati mwingine kufanya kazi hatari. Wanaume katika nyakati za kibiblia, kama vile sasa, walikuwa na maisha mafupi kwa wastani kuliko wake zao. Kwa hiyo, wajane wa kike walikuwa wengi zaidi kuliko wajane kiume.

Sababu ya pili ilikuwa ukweli kwamba wanawake mara nyingi hawakuwa na njia yoyote ya kujikimu kimaisha na watoto wao katika nyakati za kibiblia. Kuoa tena ilikuwa njia kuu ambayo mjane angeweza kupata ulinzi na kukimu mahitaji yake mwenyewe na watoto wake. Mara Kristo alipoanzisha Kanisa, Kanisa likawajibika kwa kuwajali wajane chini ya hali fulani (1 Timotheo 5: 3-10).

Suala la tatu lilikuwa kwamba kuendeleza jina ya familia ya mume lilizua wasiwasi katika utamaduni wa Kiyahudi. Matokeo yake, kama mume alikufa bila watoto kuendeleza jina lake, ndugu yake alihimizwa kuoa mjane na kumpa watoto. Wanaume wengine katika familia walikuwa na fursa pia, lakini kulikuwa na utaratibu sahihi ambapo kila mtu alikuwa na fursa ya kutimiza au kupitisha jukumu hili (angalia kitabu cha Ruthu kwa mfano). Hata miongoni mwa makuhani (ambao walipaswa kufuata kiwango cha juu), kuoa tena baada ya kifo cha mwenzi wa ndoa kuliruhusiwa. Katika hali ya makuhani, ilikuwa chini ya dhiki kwamba wao tu kuoa mjane wa kuhani mwingine (Ezekieli 44:22). Kwa hiyo, kwa kuzingatia mafundisho yote ya kibiblia juu ya suala hilo, kuoa tena baada ya kifo cha mwenzi kumeruhusiwa na Mungu.

Warumi 7: 2-3 inatuambia, " Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine." Ingawa talaka hutokea katika asilimia 50% ya ndoa leo, vidokezo vingi vya ndoa bado vina maneno "mpaka kifo kitakapotutenganisha." Kifungu hiki hakiko hasa kwa Biblia, lakini kanuni hiyo ni ya kibiblia.

Wakati mwanamume na mwanamke wanafunga ndoa, Mungu huwaunganisha kama mwili mmoja (Mwanzo 2:24; Mathayo 19: 5-6). Machoni pa Mungu, kitu pekee ambacho kinaweza kuvunja fungo ya ndoa ni kifo. Ikiwa mwenzi wa mtu anafa, mjane kike au kiume yuko huru kabisa kuoa tena. Mtume Paulo aliruhusu wajane kuoa tena katika 1 Wakorintho 7: 8-9 na kuwahimiza wajane wadogo kuoa tena katika 1 Timotheo 5:14. Kuoa tena baada ya kifo cha mwenzi wa ndoa kumeruhusiwa kabisa na Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kuoa tena baada ya kifo cha mwenzi wako?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries