settings icon
share icon
Swali

Kuna uwezekano wa kumwoa mtu asiyefaa?

Jibu


Kuna njia kadhaa za kutazama swali hili. Kusema kwamba tulioa "mtu mbaya" inaweza kumaanisha kuwa kuna mtu pekee wa "haki" ambaye tulipangiwa kuoa. Ikiwa tunoaa "mtu mbaya", basi tunaweza kuogopa tumevunja mpango wa Mungu kwa maisha yetu. Tunaweza pia kujaribiwa "kusahihisha" makosa yetu kwa njia ambazo haziheshimu Mungu. Kwa hakika tunaweza kufanya maamuzi mabaya katika ndoa na kutotii mwongozo wa Mungu hasa wa yule ambaye tunapaswa kuoa. Hata hivyo, kwa kuzingatia Ukuu wa Mungu, hatuwezi kuolewa na mtu "mbaya". Mungu ana mpango wa maisha yetu na anaweza kukomboa uchaguzi wetu usiofaa na hatimaye kuzifanya pamoja kwa manufaa (Warumi 8:28). Mara tu tumeolewa, tunatarajiwa kufanya kila kitu tunachoweza kufanya ndoa hiyo iheshimu Bwana. Hata kama ikiwa mwenzako wa ndoa ni "chaguo" baya au la, ndoa ni uhusiano wa agano. Mungu anaweza kubadilisha hata ndoa mbaya zaidi hadi uhusiano unaoletea utukufu.

Kibiblia, Mkristo anapaswa kuangalia kumwoa muumini mwingine ambaye anashiriki ahadi sawia ya kumfuata Bwana Yesu. Ndoa na asiyeamini sio chaguo kwa muumini (2 Wakorintho 6:14). Kwa hiyo, ikiwa Mkristo anaolewa na asiye Mkristo, yeye amekwisha oa mtu asiyefaa kwa kukiuka mapenzi ya Mungu.

Kuna njia nyingine za kuoa mtu asiyefaa. Kwa mfano, kuolewa na mtu ambaye ni mkatili, mchanga, mbinafsi, au hajitegemei itasababisha matatizo. Kuoa mtu ambaye hana adhabu au anaishii kwa dhambi hajatubu pia hiyo ni uchaguzi usiofaa.

Ni sababu gani ambazo hufanya watu wanoaa mtu asiyefaa? Baadhi yao huingia katika hali sumu wakiwa na imani potofu kuwa nguvu ya upendo wao peke yake itambadilisha mtu mwingine na mtu asiye na matusi, mchanga, ubinafsi, au asiyejitegema. Wengine wamepofushwa na mvuto wa kwanza kwa mwenzi na hawajui matatizo katika uhusiano wao. Wengine wamefanyishwa na mtu ambaye anaonekana kuwa jambo moja kabla ya ndoa na kisha ghafla hubadilika. Hali zingine zinahusisha wanandoa ambao hawako tayari kwa ndoa. Wanapuusa dhabihu inayohitajika ili kuishi na mtu mwingine. Bila shaka sababu katika kila hali ya kuolewa na mtu mbaya hutofautiana na ni ya kipekee kwa kila wanandoa.

Utamaduni pia unachangia katika kushawishi watu kuoa mtu asiyefaa. Jamii nyingi zimeonyesha ndoa kama mpangilio wa muda mfupi ambao unaweza kukubaliwa au kukataliwa kwa hiari. Kwa kuwa kusismua ndoa sio mpango mkubwa katika tamaduni fulani, vile vile hata kuingia. Watu wengi sana wanasema ahadi zao bila ahadi halisi kwa mwenzi wao au kwa Mungu. Katika maeneo mengi ulimwenguni, wazo linapendekewa kwamba ndoa inapaswa kukidhi mahitaji yetu yote — msisitizo ukiwa ni kutimiza mahitaji ya mtu mwenyewe, sio mahitaji ya mpenziwe. Hekima ya kawaida inasema kwamba, wakati ndoa ya wanandoa inajaribiwa au wakati mwenzi mmoja anahisi mahitaji hayajatimizwa kawaida, wanapaswa kutafuta talaka-na sheria katika maeneo mengi imefanya talaka kuwa rahisi sana. Badala ya kutatua shida zao, wanandoa wengi wanaokabiliwa na shida wanahitimisha kuwa hawapendani tena na kutamatisha ndoa.

Mara tu mtu anapofahamu kwamba yeye amoa mtu asiyefaa, basi ni nini kinafuata? Kwanza, kama muumini amekataa maagizo ya Mungu katika 2 Wakorintho 6:14 kwa makusudi, kukiri dhambi kwa Mungu ni muhimu. Kisha mwenye dhambi ambaye amesamehewa anapaswa kujitahidi kufanya hali iwe bora zaidi na kuleta uponyaji kwa uhusiano (ona 1 Wakorintho 7: 12-14; Waefeso 5: 21-33). Ikiwa hali hiyo inaleta hatari kwa mwanadnoa yeyote au kwa watoto wanaohusika, basi kuachana kunastahili. Kutafuta ushauri wa kiungu kutoka kwa mchungaji au mshauri wa ndoa ni muhimu pia. Wakati Biblia inaruhusu talaka katika hali maalum, talaka haipaswi kuwa chaguo la kwanza. Kwa Mungu hakuna kitu kisichowezekana (Luka 1:37), na anaweza kuleta uzuri kutoka majivu (Isaya 61: 3). Mkristo ambaye alifanya uchaguzi usio sahihi katika kuchagua mwenzi wa ndoa anaweza kupata kwamba Mungu anataka kugeuza ndoa mbaya kuwa nzuri (ona 1 Petro 3: 1-2). Nguvu ya Mungu inaweza kubadilisha mtu "mbaya" hadi kuwa mtu "mwema".

Mtu anawezaje kuzuia kuolewa na mtu asiyefaa? Benjamin Franklin amenukuliwa mara nyingi, "Fungua macho yako vizuri kabla ya ndoa, na yafungwe nusu baadaye," ni ushauri mzuri (Maskini Richard Almanac, Juni 1738), lakini la uzaizidizi ni kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake (Mathayo 6:33). Watu wengine hutafuta kwanza mpenzi, na utakatifu huwekwa kando. Mtu ambaye hajaolewa anapaswa kuzingatia kuwa mtu ambaye Mungu anataka awe na kujitolea kuchumbia wale tu ambao pia ni Wakristo wenye nguvu, wanaokua. Ili kuepuka makosa, ni muhimu kutii Neno (Luka 11:28), tafuta ushauri wa kiungu, omba hekima (Yakobo 1: 5), na uwe mwaaminifu kwa Mungu na wengine.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuna uwezekano wa kumwoa mtu asiyefaa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries