settings icon
share icon
Swali

Je! Ni vizuri kwa Mkristo kuchumbia au kuoa mtu ambaye si Mkristo?

Jibu


Kwa Mkristo, kuchumbia mtu ambay si Mkristo sio jambo la busara, na kuoa mmoja sio njia mbadala. Pili 2 Wakorintho 6:14 inatuambia kuwa, “msifungiwe nira pamoja na wasio amini.” Taswira ni ya ndumbe wawili ambao hawaambatani wakishiriki nira moja. Badala ya kufanya kazi pamoja, kuvuta pamoja, watakuwa wakizozana. Huku ufahamu huu hautaji ndoa moja kwa moja, uko na mchang kwa ndoa. Ufahamu huu unaendelea na kusema kuwa, hakuna upatano wowote kati ya Kristo na Berieli (Shetani). Hakutakuwa na umoja wa Kiroho katika ndoa ambayo ni kati ya Mkristo na mtu ambaye si Mkristo. Paulo anaendelea kwa kukumbusha Wakristo kuwa wao ni Hekalu la Mungu ambayo Roho Mtakatifu hukaa, ambay anazichukua mioyo yao wakati wa wokovu ( 2 Wakorintho 6:15-17). Kwa sababu ya hiyo, wanastahili kutenganishwa na ulimwengu- katika ulimwengu bali sio kutoka kwa ulimwengu-na hakuna mahali katika maisha hiyo ni muimu mbali na uhusiano wa ndoa.

Bibilia pia yasema, “Msidanganyike; Mazungumuzo mabaya huharibu tabia njema’ (1 Wakorintho 15:33). Kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na mtu asiyeamini, anaweza badilika kwa haraka na kuwa kitu kingine ambacho ni kikwazo kwa safari yako na Kristo. Tumeitwa kuwahubiria injili wenye wamepotea, sio kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao. Hakuna ubaya wowote kwa kujenga urafiki na mtu ambaye si Mkristo, lakini huo ndio umbali wastahili kufika. Kama ulikua unachumbiana na mtu asiyeokoka, kipaumbele chako cha kwanza kitakuwa, mapenzi au kumleta huyo mtu kwa Kristo? Ikiwa ulikuwa umeolewa kwa mtu ambaye si Mkristo, wawili wenu mtautunzaje wokovu wenu katika ndoa yonu? Ni namna gani ndoa nzuri inaweza jengwa na kutunzwa ikiwa mmekosa kukubaliana katika mambo muimu katika ulimwengu huu kama Bwana Yesu Kristo?

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni vizuri kwa Mkristo kuchumbia au kuoa mtu ambaye si Mkristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries