settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya unyunyizi wa Roho Mtakatifu?

Jibu


Unyunyizaji wa Roho Mtakatifu-Mungu kumimina Roho wake na kuwajaza na kushi ndani ya watu- kulitabiriwa katika Agano la Kale na kutimizwa katika siku ya Pentekote (Matendo 2). Tukio hili lilitabiriwa katika Agano la Kale: Katika Isaya 44:3 Mungu alisema, "Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu, na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka; nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako, nayo baraka yangu juu ya wazao wako." Roho mtakatifu umepewa taswira ya "maji ya uzima" ambayo yanaokoa na kubariki watu wanaoangamia. Katika siku ya Pentekote, Petro alinukuu unabii mwingine kuwa umetimiwa: "Hata itakuwa, baada ya hayo, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zenu watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono. Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile nitamimina Roho wangu…Na kila mtu atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa" (Yoeli 2:28-29,32).

Umiminiaji wa Roho Mtakatifu ulikaribisha kipindi kipya, kipindi cha kanisa. Katika Agano la Kale, Roho Mtakatifu ilikuwa karama nadra sana ambayo ilipewa watu wachache pekee, na hasa kwa kipindi kifupi. Wakati Saulo alitiwa mafuta kama mfalme wa Israeli, Roho Mtakatifu alimshukia (1 Samueli 10:10), lakini wakati Mungu aliondoa baraka yake kutoka kwa Saulo, Roho Mtakatifu alimwaacha (1 Samueli 16:14). Roho Mtakatifu alikuja kwa wakati maalum or nyakati katika maisha ya Othnieli (Waamuzi 3:10), Gideoni (Waamuzi 6:34), na Samsoni (Waamuzi 13:25; 14:6) vile vile, ili kuwawezesha kufanya mapenzi na kuwatumikia Israeli. Katika siku ya Pentekote, Roho Mtakatifu ulimiminwa kwa waumini wote katika Kristo na alikuja kuishi. Hii ilikuwa ishara ya mabadiliko makubwa katika kazi ya Roho Mtakatifu.

Kabla ya kukamatwa kakwe, Yesu alikuwa amekwisha ahidi kuwatumia wanafunzi wake Roho Mtakatifu (Yohana 14:15-17). Roho "naye anakaa ndani yenu," Yesu alisema (Yohana 14:17). Huu ulikuwa unabii wa kumiminiwa Roho, tofauti nyingine ya kipindi cha kanisa. Kumiminiwa kwa Roho Mtakatifu katika Matendo 2 inaashiria kutimia kwa maneno ya Yesu pia vile Roho Mtakatifu aliwashukia waumini wote kwa nguvu na njia iliyoonekana (sauti). Lua anasimulia tukio: "Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia" (Matendo 2:2-4). Papo hapo, Roho aliwajaza waumini na walienda katika vinjia vya Yerusalem na kumtangaza Kristo. Watu elfu tatu waliokolewa na kubatizwa siku hiyo; kanisa ikaanza (aya ya 41).

Kumiminwa kwa Roho Mtakatifu kwa wanadamu ilikuwa kukaribishwa kwa Agano Jipya, ambali likikuwa limehalalishwa na damu ya Yesu (Luka 22:20). Kulingana na maneno ya Agano Jipya, kila muumini amepewa Roho Mtakatifu (Waefeso 1:13). Tangu siku ya Pentekote, Roho Mtakatifu amekuwa akibatiza kila muumini kwa Kristo wakati wa wokovu (1 Wakorintho 12:13), anapokuja kudumu ndani ya Watoto wa Mungu milele.

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume kunayo aina tatu ya "kumiminiwa" kwa Roho Mtakatifu, kwa kikundi cha watu watatu tofauti na katika nyakati tofauti. Cha kwanza kilikuwa ni Wayahudi na waongofu kule Yerusalem (Matendo 2). Cha pili kilikuwa kikundi cha Wasamaria waumini (Matendo 8). Na cha tatu ni watu wa Mataifa walioamini (Matendo 10). Muhimu ni, Petro alikuwapo nyakti hizi zote za umimino. Mara tatu Mungu alituma Roho Mtakatifu katika ishara dhihirisho, vile kazi Kuu ya Utme ilivyokuwa ikitimizwa. Roh Mtakatifu huyo huyo aliyekuja kwa Wayahudi, Wasamaria na watu wa Mataifa katika njia ile ile mbele ya mitume hao uliweka kanisa la kwanza kuwa pamoja. Hakukuwa na kanisa la Kiyahudi, Kisamaria au Kirumi- kulikuwa na kanisa moja, "Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja" (Waefeso 4:5).

Umimino wa Roho ni tofauti na kujazwa na Roho. Umimino ulikuwa njia ya kipekee ya kuja kwa Roho Mtakatifu; ujazo unatokea wakati tunajisalimisha kwa Mungu kuongoza maisha yetu. Tunaamrishwa kuwa tujazwe na Roho (Waefeso 5:18). Kwa mjibu wa suala hili, kuna uwezekano kwa muuni aidha "kujazwa na Roho" au 'kuzima" Roho (1 Wathesalonike 5:19). Kwa njia yoyte ile, Roho Mtakatifu anabaki na waumini (kinyume na ilivyokuwa katika kipndi cha Agano la Kale, wakati Roho Mtakatifu angekuja na kuenda). Kujazwa kwa Roho huja kama matokeo ya kujusalimisha kwa mapenzi ya Mungu, na kuuzima ni matokeo ya kuasi kinyume na mapenzi ya Mungu.

Wengine bado wanatafuta "umimino" wa Roho Mtakatifu katika makundi fulani ya wat una katika mahali fulani na wakati, lakini hakuna uungwaji wa kibiblia wa urudio wa tukio kama lile la Pentekote. Kanisa limekwishaanza; mitume washaweka msingi huo (Waefeso 2:20). Wakati mwingine tunaimba nyimbo zinazomwomba Roho Mtakatifu "aje"; ukweli ni kwamba ashafika kwetu-wakati ule wa ubatizo-na mara anapokuja, hatoki tena. Umimino wa Roho ni unabii uliokamilika ambao ulikaribisha kisasai cha kanisa na Agano Jipya ambamokwamba waumini wote wamepewa Roho Mtakatifu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya unyunyizi wa Roho Mtakatifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries