Swali
Ina maana gani kumtukuza Mungu?
Jibu
"Kumtukuza" Mungu inamaanisha kumpa utukufu. Neno utukufu vile linavyohusiana na Mungu katika Agano la Kale ndani yake hubeba wazo la ukuu wa utukufu. Katika Agano Jipya, neno lililotafsiriwa "utukufu" linamaanisha "adabu, heshima, sifa na ibada." Kuyaweka mawili pamoja, tunaona kwamba kumtukuza Mungu kunamaanisha kukubali ukuu Wake na kumpa heshima kwa kumsifu na kumwabudu, kwa sababu Yeye, na Yeye peke yake, anastahili kusifiwa, kuheshimiwa na kuabudiwa. Utukufu wa Mungu ni kiini cha asili yake, na tunamtukuza Yeye kwa kutambua kuwa ni mhimu.
Swali ambalo linakuja katika akili ni kama Mungu ana utukufu wote, ambao Yeye anao, basi tunawezaje kumpa utukufu? Tunawezaje kumpa Mungu kitu ambacho ni cha chake? Funguo linapatikana katika 1 Mambo ya Nyakati 16: 28-29, "Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu. Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu." Katika aya hii, tunaona matendo mawili kwa upande wetu ambayo yanafanya kazi ya kumtukuza Mungu. Kwanza, "tunampa" au kumtukuza kwa sababu anastahili. Hakuna mtu mwingine anayestahiki sifa na ibada tunayompa kumtukuza. Isaya 42: 8 inathibitisha hivi: "Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu." Pili, tunapaswa "kuleta sadaka" kwa Mungu kama sehemu ya ibada inayomtukuza. Ni sadaka gani tunayoleta kwa Mungu ili kumtukuza?
Sadaka tunayoleta kwa Mungu tunapokuja mbele Yake katika utukufu au uzuri wa utakatifu wake inahusisha makubaliano, utii, unyenyekevu, na kurudia sifa zake au kumtukuza. Kumtukuza Mungu huanza kwa kukubaliana na kila kitu anachosema, hasa kuhusu Yeye. Katika Isaya 42: 5, Mungu anasema, "Mungu Bwana anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake." Kwa sababu ya kile Yeye aliko, mtakatifu na mkamilifu na wa kweli, sheria na amri zake ni takatifu na kamili na ya kweli (Zaburi 19: 7), na tunamtukuza kwa kusikiliza na kukubaliana nazo. Neno la Mungu, Biblia, ni Neno Lake kwetu, yote tunayohitaji kwa maisha ndani yake. Kumsikiliza na kukubaliana naye, hata hivyo, haziwezi kumtukuza Yeye isipokuwa sisi pia tunamtii na kutii amri zilizomo katika Neno Lake. "Bali fadhili za Bwana zina wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana; Maana, wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye" (Zaburi 103: 17-18). Yesu alisisitiza wazo kwamba kumtukuza na kumpenda Mungu ni moja na sawia katika Yohana 14:15: "Mkinipenda, mtazishika amri zangu."
Sisi pia tunamtukuza Mungu kwa kurudia sifa zake na matendo Yake. Stefano, katika mahubiri yake ya mwisho kabla ya kuuawa kwa ajili ya imani yake, aliisema tena hadithi ya matendo ya Mungu na Israeli tangu wakati Abrahamu aliondoka nchi yake kwa kutii amri ya Mungu, hadi ujio wa Kristo, "Mwenye haki," ambaye Israeli alimsaliti na kumuua. Tunaposema kazi ya Mungu katika maisha yetu, jinsi alivyotuokoa kutoka kwa dhambi, na kazi za ajabu anazofanya katika mioyo na akili zetu kila siku, tunamtukuza mbele ya wengine. Ingawa wengine hawataki kusikia sifa za Mungu wetu, Zaidi ya yote Yeye hupendezwa kwa hilo. Umati wa watu waliomsikia Stefano walichukia kile alichosema, wakifunika masikio yao na kukimbia kwake wakimpgiga mawe. "Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu" (Matendo 7:55).
Kumtukuza Mungu ni kupanua sifa zake-utakatifu wake, uaminifu, huruma, neema, upendo, utukufu, uhuru, nguvu, na ujuzi, kwa kutaja baadhi-kuzikalili mara kwa mara katika mawazo yetu na kuwaambia wengine juu ya asili ya pekee ya wokovu tu Yeye hutoa.
English
Ina maana gani kumtukuza Mungu?