settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje Kumtazamia Kristo?

Jibu


Katika ulimwengu wetu wa haraka, ni rahisi kupoteza kusudi letu maishani -kumwabudu Mungu. Kila mwamini, akijitahidi kuendelea kumtazamia Mungu, ana njia yake mwenyewe ya kuweka lengo hilo. Mahitaji ya kila mtu ni tofauti. Mtu mmoja anaweza kushika aya ya maandiko kila wiki; mwingine anaweza kuwa na masomo ya Biblia binafsi kila asubuhi; huku mwingine anaweza kuwa na lengo la kushiriki ujumbe wa Injili na angalau mtu mmoja kila wiki. Kila moja ya mambo haya humpa Kristo kipaumbele katika akili ya mtu.

Pia, kila moja ya shughuli hizi ina kitu sawa. Waumini wanaweza kufanya shughuli hizi ili kuweka lengo lao ambapo linapaswa kuwa. Hii ni kunyenyekea — kujisalimisha kwa Yesu Kristo, kwa Mungu. Kujisalimisha katika maisha yote: mahitaji, wasiwasi, maumivu, furaha, sifa. Kujisalimisha kimwili, hisia, akili, na kiroho. Fikiria mistari ifuatayo: Warumi 12: 1: "Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu.

Je! haya ni mengi sana kuuliza unapofikiria yote ambayo amekutendea? " Luka 9: 23-24: "Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. " Waroma 6:13:" wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.

Unapoyasalimisha maisha yako haina budi kuwa na imani. Ni kuwa na matumaini kwamba Mungu anayajali maslahi yako. Ni kuamini kwamba Neno lake linaweza kuaminika. Inatumaini kwamba mahitaji yako yote yatimizwa. Unapojisalimisha unachukua hatua ya kutojitegemea ili upate kumtazamia Kristo, na hio inajionyesha kwa kutii. Mchungaji Rick Warren wa Kanisa la Saddleback katika Msitu wa Ziwa, California, anaandika, "Kujisalimisha siyo njia bora ya kuishi, ni njia pekee ya kuishi, hakuna kitu kingine chochote kinachofanya kazi.Njia zingine zote husababisha kuchanganyikiwa, kukata tamaa na uharibifu wa mtuu mwenyewe." Hakuna njia bora ya kumtazamia Bwana kama muumini kuliko kuyasalimisha kikamilifu maisha yako kwa Bwana na Mwokozi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje Kumtazamia Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries