settings icon
share icon
Swali

Kwa nini kumtafuta Mungu ni muhimu?

Jibu


Katika barua ya Paulo kwa kanisa huko Roma, yeye ananukuu taarifa ya kushangaza kutoka Zaburi: "Hakuna mtu anayeelewa; wala anayemtafuta Mungu" (Warumi 3:11). Jinsi gani, Paulo na Daudi hapo mwanzoni, walitoa tamko kubwa kama hilo? Je, kati ya wote ambao wamewahi kuishi, hakuna hata mmoja amewahi kumtafuta Mungu? Mabilioni ya watu wametafuta mungu fulani, lakini mara zote hawakumtafuta Mungu wa ukweli.

Ukweli huu unaungana moja kwa moja na dhambi ya Adamu na Hawa iliyosababishwa udanganyifu wa shetani. Katika historia ya mwanadamu, udanganyifu unaoenezwa na shetani hivi kwamba mwanadamu halisi anaweza tu kutambua vipande vidogo kuhusu ukweli wa Mungu. Matokeo yake ni kuwa maoni yetu kuhusu Mungu yanatiwa doa. Wakati Mungu anapochagua kujidhihirisha kwetu basi vipande hivyo vinaweza kuleta maana na macho yetu yanafungukuka kuona ukweli. Basi, kwa kweli kumtafuta Mungu kunawezekana.

Yesu anatuambia katika Yohana 17:3, " Na uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma." Hapa Yesu anatuambia kwamba kuendelea kumtafuta Mungu, kutamani kumjua zaidi, ndio kiini cha maisha ya kweli na uzima wa milele. Mawazo muhimu ambayo akili zetu ziwaweza kuwa nayo ni mawazo ya Mungu, kwa sababu yataamua ubora na mwelekeo wa maisha. Kumtafuta Mungu basi ni jukumu linaloendelea n ani pendeleo la waKristo wote.

Lakini pia tunajua kumtafuta Mungu kawaida sio jambo rahisi kufanya, sio kwa sababu Mungu hafahamiki, lakini ni kwa sababu akili zetu zimejawa na fikra potovu na udanganyifu uliopandwa na shetani na kuimarishwa na tamaduni, bila kusahau asili ya mioyo yetu yenye dhambi na udanganyifu wa dhambi (Yeremia 17:9; Yakobo 1:13-15). Lakini habari njema ni kwamba amani hizi potovu zinaweza kuondolewa kwa kumjua Mungu na kukua katika uhusiano wetu pamoja naye. Jambo hili huanza wakati tunamgeukia kwa wokovu na kuweka Imani yetu kwake Yesu Kristo. Tunapookoka, tunapokea Roho Mtakatifu amabaye anatusaidia kumjua Mungu na hata hubadilisha mioyo yetu kutaka kumtafuta (Waefeso 1:!3-14); Wafilipi 1:6;2:12-13; Warumi 8:26-30). Warumi 12:2 inashauri, "Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu." Tunajifunza ukweli juu ya Mungu na kumtafuta kupitia kusoma Neno lake (Biblia). Tunamtafuta Mungu kupitia maombi na katika nyakati za ibada. Tunamtafuta Mungu kibinafsi na kwa ushirika. Kushiriki na waumini wengine katika Yesu ambao pia wanamtafuta Mungu ni muhimu kwa kutusaidia kuzidi kumtafuta ( Waebrania 10:24-25).

Mambo ya Nyakati ya PilI 15:2-4 inatupa mafunzo. Kifungu hiki kiliandikwa zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita kwa watu kama sisi: "Naye Nabii Azaria akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; Bwana yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi. Basi tangu siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati;lakini walipomgeukia Bwana, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao."

Maagizo yao yalikuwa rahisi: Wakati walimtafuta Mungu kwa dhati, mambo yalikwenda vizuri, lakini wakati hamu yao ya kumtafuta ilipungua na kukoma kabisa mwishowe, dunia yao ilisambaratika. Dhambi iliongezeka, maadili yakapungua, na mawasiliano na Mungu yakakoma. Maagizo kwa watoto wa Mungu wakati huo ni wazi kwetu leo: "Mkimtafuta Mungu wenu, nanyi mtampata." Kanuni hii inarudiwa katika maandiko (Kumbukumbu la Torati 4:29; Yeremia 29:13; Mathayo 7:7; Matendo ya Mitume 17:27; Yakobo 4:8). Wazo hii ni kwamba wakati tunapomkaribia Mungu, yeye anajidhihirisha kwetu. Mungu hajifichi kutoka kwa moyo unaomtafuta.

"Kisha kutoka humohumo nchini mtamtafuta Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nanyi mtampata kama mkimtafuta kwa moyo wote na roho yote." (Kumbukumbu la Torati 4:29)

"Mtanitafuta na kunipata. Mtakaponitafuta kwa moyo wote." (Yeremia 29:13)

"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa. (Mathayo 7:7)

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini kumtafuta Mungu ni muhimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries