Kwa nini kumngojea Mungu ni ngumu sana?


Swali: "Kwa nini kumngojea Mungu ni ngumu sana?"

Jibu:
Kumngojea Mungu sio ngumu tu; wakati mwingine inaonekana haiwezekani. Tunataka vitu kufanyika wakati wetu wenyewe, kulingana na mipango yetu. Lakini Mungu hafanyi kazi kwa ratiba zetu, na tunapotarajia kwamba Yeye atatenda huwa tunakata tamaa. Mungu ana mtazamo mkubwa zaidi wa matukio ya maisha, na mtazamo wake, mipango, na ratiba ni kamili na takatifu, kwa sababu Yeye ni mkamilifu na mtakatifu. Mtunzi hutuambia " Njia ya Mungu ni kamili" (Zaburi 18:30). Ikiwa njia za Mungu ni "kamilifu," basi tunaweza kuamini kwamba chochote anachofanya-na wakati wake pia ni kamilifu. Tunapokuja kuelewa ukweli huo, kumngojea Mungu inakuwa sio ngumu sana, tunasubiri kwa furaha.

Ahadi za Mungu ni wazi juu ya suala hili — ikiwa tunamngojea Mungu, atafanya upya nguvu zetu (Isaya 40:31). Lakini sisi ni wanadamu na tunaishi katika utamaduni ambao unahitaji kila kitu sasa hivi au hata jana. Ndiyo sababu kumngojea Mungu ni vigumu. Wakati mwingine, sala tunayoinua kwa Bwana wa Majeshi yanajibiwa mara moja, na hiyo inatuhimiza kuendelea kuamini na kujiamini. Hata hivyo, wakati mwingine kwa muda, Bwana hujaribu imani yetu, na wakati huo tunaweza kutatizika. Hiyo ni wakati mambo yanaweza kuwa magumu na wakati tunapojiuliza kama Bwana kweli anasikiza sala yetu.

Mtume Paulo anahimiza kanisa la Filipi wasiwe na wasiwasi juu ya chochote (Wafilipi 4: 6). Muumini anapokuwa na wasiwasi anaonyesha ukosefu wa imani na hio inauzunisha Mungu, si tu kwa sababu hataki sisi tuwe na wasiwasi kwa chochote, bali pia kwa sababu anajua wasiwasi wetu hutokana na ufahamu usio kamilifu kumuhusu.

Ukuu wake Mungu ni kipengele muhimu cha asili yake na tabia yake, na sifa ambayo itatusaidia sisi kumngojea kwa uvumilivu kamili. Ukuu wa Mungu hufafanuliwa kama udhibiti wake kamili na wa jumla juu ya kila kiumbe, tukio, na hali kila wakati katika historia. Bila kushawishiwa na yeyote, akijitegemea, kabisa, Mungu hufanya kile anachopenda, tu kama anavyopendeza, na hakuna chochote kinachoweza kumzuia: " nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote. "(Isaya 46:10). Mara tunapofahamu hivyo, tunasubiri Mungu wetu kamili kufanya kazi na kutenda wakati wake kamilifu. Haituwezeshi kusubiri kwa uvumilivu pekee, lakini pia inatuwezesha kusubiri kwa uaminifu.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini kumngojea Mungu ni ngumu sana?