settings icon
share icon
Swali

Kumpinga Kristo ni nini?

Jibu


Yohana ya kwanza 2:18 inaongelelea kuhusu kumpinga Kristo: " Watoto wapendwa, huu ni wakati wa mwisho. Na kama mlivyokwisha kusikia kwamba yule mpinga Kristo anakuja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuja, kwa hiyo tunajua kuwa huu ni wakati wa mwisho." Neno kumpinga Kristo limetumika mara saba katika maandiko, mara mbili kwa hiki kifungu cha Yohana ya kwanza 2:18 na pia Yohana ya kwanza 2:22; 4:3; na mara mbili katika Yohana ya pili 1:7. Je, hii kumpinga Kristo yenye mtume Yohana anaongelelea ni nini?

Maana ya maneno Kumpinga-Kristo ni kuenda "kinyume na Kristo." Jinsi mtume Yohana ameandika katika Yohana ya kwanza na ya pili, mpinga Kristo anamkataa Baba na Mwana ( Yohana ya kwanza 2:22), hamtambui Yesu (Yohana ya kwanza 4:3), na anakataa kwamba Yesu alikuja kwa mwili ( Yohana ya pili 1:7). Wapinga Kristo wengi wamekua vile Yohana ya kwanza 2:18 inasema. Lakini pia kuna wapinga Kristo amabao wanakuja.

Wataalam wengi wa unabii wa kibiblia wanaamini kuwa kumpinga Kristo itakua mfano halisi wa kuwa kinyume na Kristo. Katika nyakati za mwisho/saa ya mwisho, mtu atajitokeza kumpinga Kristo na wafuasi wake kuliko mtu yeyote kwenye historia. Vile vile kudai kuwa masihi wa ukweli, mpinga Kristo atatafuta utawala wa ulimwengu na kujaribu kuwapotosha na kuwaangusha wafuasi wa Yesu Kristo na taifa la Israeli.

Marejeleo mengine ya Kibiblia kuhusu kumpinga kristo ni kama yafuatayo:

Ule mfalme wa kujisifu na kuweka sheria Katika Danieli 7 ambaye anawatesa Wayahudi na kujaribu " kubadilisha nyakati na sheria zao" ( mstari wa 25).

Kiongozi ambaye alitengeneza agano la miaka saba na waisraeli alafu akalivunja katika Danieli 9.

Mfalme ambaye anaweka chuki ya kujitenga katika Mariko 13:14 ( pia Danieli 9:27).

Mtu mwenye anaasi sheria katika Watheseloniki ya pili 2:1-12.

Mpanda farasi nyeupe ( ambayo inawakilisha kudai kwake kuwa yeye ni mtu wa Amani) katika Ufunuo 6:2.

Mnyama wa kwanza-kutoka baharini- katika Ufunuo 13. Huyu mnyama anapokea nguvu kutoka kwa shetani na kusema "maneno ya kujigamba na kumkufuru Mungu" (mstari wa 5) na kuwapiga vita na kuwashinda watu wa Mungu (mstari wa 7).

Uzuri, mpinga Kristo/mnyama, pamoja na nabii wake wa uongo watatupwa katika bahari ya moto penye wataishi milele kwa mateso (Ufunuo 19:20; 20:10).

Kumpinga Kristo ni nini? Kwa ufupi, mpinga Kristo ni masihi wa uongo wa nyakati za mwisho ambaye anatafuta, na pengine kufanikiwa, utawala wa ulimwengu ili aweze kuharibu Israeli na wafuasi wa Yesu Kristo.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kumpinga Kristo ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries