settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kumpenda Bwana kwa moyo wako wote, roho, akili, na nguvu?

Jibu


"Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote"(Kumbukumbu la Torati 6: 4-5). Hii inajulikana kama Shema, iliyotokana na neno la kwanza "kusikia" kwa Kiebrania. Wayahudi wa kisasa wanafikiria kukalili Shima kila jioni na asubuhi kuwa moja ya kazi zao takatifu zaidi. Ilionyeshwa na Yesu kuwa "amri kubwa zaidi katika Sheria" (Mathayo 22: 36-37).

Amri hii inaonekana haiwezekani kuitii. Hiyo ni kwa sababu, katika hali ya asili ya mwanadamu, haiwezekani. Hakuna ushahidi mkubwa wa kutoweza kwa mwanadamu kutii Sheria ya Mungu kuliko amri hii moja. Hakuna mwanadamu aliye na asili iliyoanguka anaweza kumpenda Mungu kwa moyo wake wote, roho na nguvu zake masaa 24 kwa siku. Kibinadamu haiwezekani. Lakini kutotii amri yoyote ya Mungu ni dhambi. Kwa hiyo, hata bila kufikiria dhambi tunazofanya kila siku, sisi sote tumehukumiwa na kutokuwa na uwezo wa kutimiza amri hii moja. Hii ndio sababu Yesu aliwahi kuwakumbusha Mafarisayo kwa kukosa uwezo wao wa kuzingatia Sheria ya Mungu. Alikuwa akijaribu kuwafanya waweze kuona uharibifu wao wa kiroho na hivyo kumhitaji Mwokozi. Bila ya usafisho wa dhambi ambao Yeye hutoa, na kuwepo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ambaye anaishi ndani ya mioyo ya walio kombolewa, kumpenda Mungu kiwango chochote huwa ngumu.

Lakini, kama Wakristo, tumejitakasa kutoka kwa dhambi na tuna Roho. Basi, tunaanzaje kumpenda Mungu kwa njia tunayotakiwa? Kama vile mtu katika Mariko 9:24 alimwomba Mungu amsaidie kwa kutokuamini kwake, ndivyo tunapaswa kumwomba Mungu atusaidie katika maeneo ambayo hatupendi kwa moyo wetu wote, roho, akili na nguvu zetu zote. Ni nguvu yake kwamba tunahitaji kufanya yale hayawezekani kwetu, na tunaanza kwa kutafuta na kuimarisha nguvu hiyo.

Katika hali nyingi, upendo wetu na pendo letu kwa Mungu huongezeka zaidi wakati unapoendelea na kusonga. Hakika, Wakristo wachanga na wapya waliokolewa wanajua sana upendo wa Mungu na upendo wao kwa Yeye. Lakini ni kupitia ushahidi wa uaminifu wa Mungu wakati wa mapambano na majaribio kwamba upendo wa kina kwa Mungu unakua na kukua. Baada ya muda, tunashuhudia huruma, rehema, neema, na upendo wake kwetu, vile vile chuki yake kwa dhambi, utakatifu wake, na haki yake. Hatuwezi kumpenda mtu tusiyemjua, kwa hivyo kumjua lazima iwe kipaumbele cha kwanza. Wale wanaomtafuta Mungu na haki yake, ambao huchukua amri ya kumpenda zaidi ya yote, ni wale ambao wamgubikwa na vitu vya Mungu. Wana hamu ya kujifunza Neno la Mungu, nia ya kuomba, hamu ya kumtii na kumheshimu Mungu katika mambo yote, na nia ya kuwaambia wendinge kuhusu Yesu Kristo. Ni kwa njia ya taaluma hizi za kiroho upendo wa Mungu unakua na kukomaa kwa utukufu wa Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kumpenda Bwana kwa moyo wako wote, roho, akili, na nguvu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries