settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya kukua kiroho?

Jibu


Kukua kiroho ni njia moja ya kumfanana Kristo, na kutubadilisha kuwa mfano wake. Kukua kiroho imeelezwa vizuri sana katika 2 Petero 1:3-8, ambayo yatuambia kwamba kwa nguvu za Mungu “tuko na kila kitu tutakacho” kuishi maisha ya kiungu, ambayo ndio lengo la kukua kiroho. Kumbuka kwamba chenye tunahitaji kinakuja “kupitia ufahamu wetu kwake,” ambao ndio funguo wa kupata chochote tunachohitaji. Ufahamu wetu Mungu watoka kwa neno lake, ambalo tumepewa kwa kutujenga na kukua.

Kuna ratiba mbili katika Wagalatia 5:19-23 yataja “matendo ya mwili.” Haya ni mambo ambayo yanatambulisha maisha yetu kabla tuje kwa Kristo kwa wokovu. Matendo ya mwili ni zile kazi ambazo twastahili kuzikiri, kutubu, na kwa uzaidizi wa Mungu tutazishinda. Tunapoanza kuhisi ukuaji wa kiroho, chache ya “matendo ya mwili” yatakuwa wazi katika maisha yetu. Mpangili wa pili ni “matunda ya Roho Mtakatifu” (aya 22-23). Hizi ndizo zinastahili kutambua maisha yetu kwa vile tumekwisha pata wokovu katika Yesu Kristo. Kukua kiroho unatambulika kwa matunda ya Roho Mtakatifu yanapoendele kuonekana yakiozengezeka katika maisha ya Mkristo.

Wakati ubadilisho wa wokovu unafanyika, ukuaji wa kiroho unaanza. Roho Mtakatifu unakaa ndani yetu (Yohana 14:16-17). Sisi ni viumbe vipya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17). Utu wa kale umebadilishwa na utu upya (Warumi 6-7). Ukuaji wa kiroho ni kitu kinachoendelea katika maisha yetu ikitegemea vile tanavyolisoma na kulitumia neno la Mungu (2 Timotheo 3:16-17) na mienendo yetu katika roho (Wagalatia 5:16-26). Tunapotafuta kukua kiroho, lazima tuombe kwa Mungu na kuuliza hekima kuhusu zile sehemu Mungu anataka tukue. Tunaweza kumuuliza Mungu aiongeze imani yetu na ufahamu wetu kwake. Mungu anataka sisi tuwe kiroho, na amatupa yote tunayostahili ili tuhisi uaji kiroho. Tukisaidiwa na Roho Mtakatifu tutashinda dhambi na kumfanana mwokozi wetu Bwana Yesu Krosto.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya kukua kiroho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries