settings icon
share icon
Swali

Ni sababu zipi hasa za kukosa kanisa?

Jibu


Watu wengi wana ufahamu usiofaa au usio wa kibiblia wa kuhudhuria kanisa. Watu wengine wanahisi kuhudhuria kanisa kumebanwa katika sheria – lazima wahudhurie kila wakati kuna aina yoyote ya huduma au mkutano, la sivyo kuna athari ya ghadhabu ya Mungu. Watu wengine huwa na hisia za hatia wakati wowote wanapokosa huduma ya Jumapili asubuhi kwa sababu yoyote ile. Kwa kusikitisha, baadhi ya makanisa huhimiza hisia hizi za hatia kwa kuweka shinikizo nyingi kwa watu. Ilhali kutotilia maanani kanisa au kuepuka kanisa kwa hiari kunaweza kuashiria tatizo katika afya ya kiroho ya mtu, ni muhimu kuelewa kwamba ubora wa uhusiano wa mtu na Mungu hauashiriwi kwa mara ngapi yeye yupo kanisani. Upendo wa Mungu kwa watoto Wake hautegemei idadi ya mara wanahudhuria huduma rasmi.

Hakuna shaka kwamba Wakristo, wafuasi wa Yesu Kristo, wanapaswa kuhudhuria kanisa. Inapaswa kuwa tumaini la kila Mkristo kuabudu pamoja (Waefeso 5: 19-20), kushiriki na kuhamasisha Wakristo wengine (1 Wathesalonike 5:11), na kufundishwa Neno la Mungu (2 Timotheo 3: 16-17). Kusikia Neno ndio hutoa imani (Warumi 10:17). Na kukusanyika pamoja na waumini wengine ni amri (Waebrania 10: 24-25); tunahitaji kweli kila mmoja. Kama vile Mungu ampenda mtoaji mwenye furaha (2 Wakorintho 9: 7), hivyo ndivyo anavyo furahishwa na anayehudhuria kanisa kwa furaha.

Kuhudhuria kanisa kunapaswa kuwa mojawapo ya vipaumbele katika maisha ya Kikristo. Kuwajibika katika kanisa la mtu ni muhimu. Basi kuna sababu zipi hasa za kukosa kanisa? Haiwezekani kutoa orodha ambayo itafanya kazi kwa kila mtu. Bila shaka, imekubalika kukosa kanisa wakati mtu ni mgonjwa. Lakini, katika maeneo mengine, suala hutokea kwa mtazamo wa mtu na motisha. Ikiwa msukumo wa mtu kwa kukosa kanisa ni heri kumtumikia Bwana mahali pengine, kukidhi mahitaji fulani, au kutimiza wajibu uliowekwa na Mungu, basi hakuna kitu kibaya kwa kukosa huduma ya kanisa. Kwa mfano, polisi wa zamu, hatarajiwi kupuuza wito ili kuchukua nafasi yake kanisani. Lakini kama msukumo wa mtu kukosa kanisa ni kutimiza tamaa za mwili, kufuata visivyo vya haki, au tu kuepuka ushirika wa Kikristo, basi kuna tatizo.

Kila hali lazima ikaguliwe kibinafsi na kwa uaminifu. Je, imekubalika kamwe kukosa kanisa ili kuhudhuria tukio la michezo? Ndio, inategemea motisha na mtazamo wa mtu. Je, na kukosa kanisa wakati wa likizo? Tena, inategemea motisha na mtazamo wa mtu. Tunataka kuepuka usheria; hatuokolewa kwa kuhudhuria kanisa ila kwa neema. Hata hvyo, Mkristo anapaswa kutamani kuhudhuria kanisa ili kujifunza kuhusu ukuu wa zawadi ya Mungu ya wokovu, kujifunza Zaidi jinsi ya kuwa kama Kristo, na kupata fursa ya kuwatumikia wengine.

Kwa kuchunguza nia zetu za kukosa kukosa, tunapaswa pia kuchunguza nia zetu za kuhudhuria kanisa. Je, tunahudhuria kanisa ili tujifanye kiroho? Kutangamana na fursa za kibiashara? Au, huwa tunahudhuria kwa sababu ya dhana ya kisheria ambayo inasema kuwa mara nyingi tunapitia milango ya kanisa, ndivyo Mungu anafurahi zaidi na sisi? Ni kweli kwamba kuna watu wengi ambao huhudhuria kanisa mara kwa mara lakini hawana uhusiano mzuri na Bwana. Ikiwa kuhudhuria kwako kanisa hakuna maana zaidi kuliko kukaa ukiboeka na kutokuwa na umakinifu kusikiza wakati wa kuimba na mahubiri, na kisha kuondoka punde tu baada ya huduma kumalizika, basi afadhali hata ungekosa kanisa, kwa vile hukupata kitu chochote kutoka kwa huduma wala hukuchangia chochote.

Tunapaswa kuhudhuria kanisa ili tuweze kushirikiana na wengine ambao pia wamepata neema ya ajabu ya Yesu Kristo. Tunapaswa kuepuka kukosa kanisa iwezekanavyo, kwa sababu tunatambua umuhimu wa kusikia Neno la Mungu, kulitumia katika maisha yetu, na kulishiriki na wengine. Tunapaswa kuhudhuria kanisa, sio kukusanya pointi za ziada za kiroho, bali kwa sababu tunampenda Mungu, tunawapenda watu wake, na tunalipenda Neno Lake. Kila Mkristo anapaswa kujaribu kuhudhuria kanisa mara kwa mara. Hata hivyo, kukosa kanisa kwa sababu nzuri kamwe sio dhambi au kitu ambacho kinapaswa kusababisha hisia za hatia.

Mungu anazijua nyoyo zetu. Mungu havutiwa na mtu tu kwa sababu anahudhuria kila huduma. Nia ya Mungu ni kutujenga katika Kristo, na mbinu yake katika kisasi hiki inahusisha kanisa la nyumbani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni sababu zipi hasa za kukosa kanisa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries