settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kukimbia kutoka kwa majaribu?

Jibu


Kukimbia kutoka kwa majaribu ina maana kwamba tunatambua kuwa ni adui na tunaendena njia nyingine, bila kusita wala kulegeza masharti. Wakorintho wa Kwanza 6:18 inasema, “Ikimbieni zinaa. dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe.” Ingawa jaribu hilo sio dhambi, usherati huanza na kishawishi cha kufanya ngono nje ya mipaka ya Mungu. Tusipokimbia jaribu hilo, hatua hufuata upesi.

Mfano bora na halisi wa kibiblia wa mtu anayeyakimbia majaribu unapatika katika Mwanzo 39 wakati kijanaYusufu mwanawe Yakobo, alilengwa na mke wa bwana wake kwa ajili ya uzinzi. Alimshawishi siku baada ya siku, lakini Yusufu alishikilia msimamo wake na kukataa majaribu yake. Hakukataa kufanya mapenzi naye pekee, bali kwa hekima alikataa “kukaa karibu naye” (Mwanzo 39:10). Lakini siku moja wakati hakukuwa na mtu yeyote kwa nyumba, alimshika Yusufu na kumvuta kwake, akajaribu kumshawishi: “Mke wa Potifa akashika vazi Yusufu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yusufu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia” (aya ya 12). Huo ni mfano bora wa kuyakimbia majaribu. Yusufu hakusimama hapo na kubishana au kujipa muda wa kutafakari upya. Alitoroka.

Kwa kawaida tunatoroka hatari. Jengo tulimo linaposhika moto, tunakimbilia mahali salama zaidi. Wakati kimbunga kinakaribia kutua, tunakimbia pwani. Kwa bahati mbaya, watu wengi wanapoona majaribu yanakuja, hawakimbii. Badala ya kukimbia majaribu, wao hujishughulisha nayo. Huipotosha, huiahirisha, au kuichambua; wengine wanaikumbatia. Je, hii inaweza kuwa ndio sababu ya watu wengi hawagundui hatari iliyomo katika majaribu? Tunaonekana kujishughulisha zaidi na hatari za kimwili zinazotishia mwili kuliko tunavyojali hatari za kiroho zinazotishia nafsi.

Warumi 13:14 inasema, “Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, wala msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi.” Kuuwezesha mwili ni kinyume na kukimbia majaribu. Tunauwezesha mwili wakati tunakumbatia mambo ambayo hutuelekeza kwa dhambi na hakika kuwezesha dhambi. Wale wanaouwezesha mwili ni kama aina ya yule mzazi mpotovu anafumbia macho tabia mbaya ya mtoto wake na kukidhi kila matakwa yake. Tunapojiruhusu kubaki katika hali zenye majaribu badala ya kuzikimbia, tunaweka imani yetu kiupumbavu katika mwili. Tunaamini uongo kwamba mwili wetu wa dhambi kwa namna fulani utapata nguvu ya kupigana mwishowe. Kisha tunashutuka na kuaibika wakati badala ya kupinga, tunakubali.

Mungu hutuoa nguvu na ujasiri kwa mtoto Wake yeyote ambaye ataishi akiwa amejisalimisha kwa mapenzi Yake (2 Wathesaloniki 2:16-17; Waebrania 12:10-12). “Jina la Bwana ni ngome imara, wenye haki huikimbilia na kuwa salama” (Mithali 18:10). Tumeamriwa katika Maandiko yote kusimama imara na kupinga mbinu za shetani (Waefeso 6:10-18; Yakobo 4:7; 1 Petro 5:9). Mitego ya Shetani ni mingi na ni tofauti na kwa kawaida huanaza na wazo au hali inayojaribu. Njia moja ya kumpinga shetani ni kukimbia tunapopata majaribu ya kwanza.

Tunapokimbia kutoka kwa majaribu, kiasili huwa tunakimbilia kitu kingine, na Paulo anatuambia kitu hicho kinapaswa kuwa ni: “Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi” (2 Timotheo 2:22). Hekima hutambua hatari katika majaribu na kutusihi tuikimbie. “Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele kama kipofu nayo ikamtesa” (Mithali 22:3).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kukimbia kutoka kwa majaribu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries