settings icon
share icon
Swali

Mtazamo wa swala la kujiua kikristo ni nini? Biblia inasemaje juu ya kujiua?

Jibu


Kulengana na Biblia, kujiua si kigezo cha kukufanya uingie mbinguni. Mtu asiyeokoka akijiua huwa amejipeleka moja kwa moja katika ziwa la moto. Mtu huyu atapelekwa huko kwa kukataa kwake wokovu kupitia Yesu, si kwa sababu alijiua. Biblia inataja watu wanne waliojiua: Sauli (samueli wa kwanza 31:4), Ahithofeli (samueli wa pili 17:23), Zimri (wafalme wa kwanza 16:18), na Yuda (Mathayo 27:5). Kila mmoja wao alikuwa mwovu na mwenye dhambi. Biblia inachukulia kujiua sawa na kuua – na hivyo ndivyo ilivyo – kujiua mwenyewe. Mungu ndiye ni aamue lini na vipi mtu afe. Kuchukua jukumu hilo mkononi mwako kibiblia ni kufuru kwa Mungu.

Je, biblia inasemaje juu ya mkristo akijiua? Siamini ya kwamba mkristo anayejiua atapoteza wokovu wake aende motoni. Biblia inatufundisha ya kuwa kuanzia wakati mtu anapomwamini kristo ana usalama wa milele (Yohana 3:16). Kulengana na biblia wakristo wanauhakika kuwa wana uzima wa milele haijalishi kutatokea nini. “Haya mambo nimewaandikia ninyi wenye kuamini juu ya mwana wa mungu, ili mjue mna uzima wa milele na mdumu katika kumwamini mwana wa mungu” (Yohana wa kwanza 5:13). Hakuna kinachoweza kumtenganisha mkristo na upendo wa mungu! “kwa kuwa nimeshawishika si mauti wala uzima, wala malaika, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo wala yaliyojuu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa mungu ulio katika kristo Yesu Bwana wetu” (warumi 8:38-39). Kama kiumbe kinginecho chote hakina uwezo wa kumtenganisha mkristo na upendo wa Mungu basi hata “mkristo anayejiua,” “kiumbe kilichoumbwa,” kujiua kwake hakumtenganishi na upendo wa Mungu.Yesu alikufa kwa ajili ya dhamhi zetu zoto … na kama mkristo halisi, katika mapambano ya kiroho akiwa mnyonge, akijiua – hiyo itakuwa ni mojawapo ya dhambi alizozifia Yesu.

Hii si kwamba kujiua ni dhambi ndogo machoni pa Mungu. Kulengana na biblia kujiua ni kuua na kila mara ni kosa Mimi pia ningekuwa na shaka na imani ya mtu anayejidai kuwa mkristo halafu ajiue. Hakuna linalompa haki yeyote anayejiua. Wakristo huitwa waishi maisha yao kwa ajili ya Mungu –mipango ya kufa kwake iko mikononi mwa Mungu mfano wa kujiua wa mkristo ungekuwa kutoka kitabu cha Esta. Katika uajemi walikuwa na sheria ya kwamba yeyoto mbele ya mfalme bila kualikwa na mfalme angeuawa isipokuwa mfalme aliponyosha fimbo yake kumwelekea mtu huyo – kumaanisha huruma. Kujiua kwa mkristo ni sawa na kujilazimisha kuenda mbele ya mfalme mwenyewe bila kungoja mfalme akuite. Atanyosha fimbo yake kwako kuhifadhi uzima wako wa milele lakini haimaanishi kuwa anafurahishwa nawe. Mfano mzuri wa mwenye kujiua katika biblia, wakorintho wa kwanza 3:15, unaonyesha linalofanyika mkristo anapojiua: “yeye mwenyewe ataokolewa, lakini sawa na mtu mwenye kutoroka kupitia ndani ya ndimi za moto.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mtazamo wa swala la kujiua kikristo ni nini? Biblia inasemaje juu ya kujiua?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries