settings icon
share icon
Swali

Je Mkristo ana mtazamo upi kwa kujitukuza?

Jibu


Wengi hufafanua kujitukuza kama “Hisia zenye thamani fulani zenye msingi kwa ujuzi wao, utimilifu, hali, rasilimali za kifedha,au kujitokeza.” Aina hii ya kujithamini kunaweza kusababisha mtu kujisikia huru na mwenye kiburi na kujiingiza katika kujiabudu , ambayo huchosha tumaini letu kwa Mungu. Yakobo 4: 6 inatuambia kwamba "Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. "Ikiwa tutaamini urithi wetu wa duniani, hatutaepuka kuachwa na wazo la thamani lenye misingi kwa kiburi. Yesu alituambia," Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya." (Luka 17:10).

Hii haimaanishi kwamba Wakristo hawapaswi kutukuza. Ina maana tu kwamba wazo letu la kuwa mtu mzuri haipaswi kutegemea kile tunachofanya, lakini badala yake kile tulicho katika Kristo. Tunahitaji kujinyenyekeza mbele yake, na yeye atatuheshimu. Zaburi 16: 2 inatukumbusha, "Nimemwambia Bwana, ndiwe Bwana wangu; sina wema ila utokao kwako." Wakristo wanaafikia kujithamini na tukuzo kwa kuwa na uhusiano wa haki na Mungu. Tunaweza kujua tuna thamani kwa sababu ya bei ghali Mungu alitulipia kupitia kwa damu ya Mwanaye, Yesu Kristo.

Kwa maana nyingine, kutojitukuza ni kinyume cha kiburi. Kwa maana nyingine, kutojitukuza ni aina ya kiburi. Baadhi ya watu hawajithamini kwa sababu wanataka watu wawahurumie,wajishughulishe nao, ili kuwafariji. kujitukuza kunaweza kukiriwa kuwa "nitazame mimi" tu kama vile kiburi. Inachukua tu njia tofauti ili kufika hatima hiyo hiyo, kwamba ni, ufyonzaji nafsi ,tamaa isiyotulizika, na ubinafsi. Badala yake, tusiwe na ubinafsi, tusijifie wenyewe, na tuvute upande makini yoyote tuliyopewa kwa Mungu mkuu ambaye alituumba na anayetulinda.

Biblia inatuambia kwamba Mungu alitupa thamani wakati alitununua tuwe watu wake mwenyewe (Waefeso 1:14). Kwa sababu hii, tu Yeye anastahili heshima na sifa. Wakati tunajitukuza kiafya, tutajithamini sisi wenyewe ya kutosha ili tusishiriki katika dhambi inayotufanya watumwa. Badala yake, tunapaswa kujiendesha kwa unyenyekevu,tukiwaza wengine kuwa bora kutuliko sisi wenyewe (Wafilipi 2: 3). Warumi 12: 3 inatuonya, "Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtukiasi cha imani."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je Mkristo ana mtazamo upi kwa kujitukuza?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries