Swali
Biblia inasema nini kuhusu kujisamehe mwenyewe?
Jibu
Kamwe Biblia hazungumzii juu ya wazo la "kujisamehe mwenyewe." Tunaambiwa kuwasamehe wengine wakati wanatukosea na kutafuta msamaha. Tunapoomba msamaha kwa Mungu kwa kuzingatia kwamba Kristo tayari amelipa kwa ajili ya dhambi zetu na kumtegemea Yeye kama Mwokozi na Bwana, Yeye anatusamehe. Ni rahisi tu hivyo (1 Yohana 1: 9). Hata hivyo, hata kama sisi tuko huru kutoka utumwa wa dhambi (kama ilivyoelezwa katika Warumi sura ya 6-8), tunaweza bado kuchagua kuwa na tabia za mtu amabaye hajawekwa huru kutoka utumwa wa dhambi. Vivyo hivyo, pamoja na hisia za hatia tunaweza kukubali ukweli kwamba tumesamehewa katika Kristo, au tunaweza kuamini uongo wa shetani kuwa bado tuna hatia na tunapaswa kujisikia kama wenye hatia.
Biblia inasema kwamba wakati Mungu anapotusamehe, "hatokumbuka dhambi zetu tena" (Yeremia 31:34) Hii haimaanishi kuwa Mungu anayejua yote husahau kwa sababu Yeye hutusamehe. Badala yake, Yeye huchagua kutokumbuka dhambi zetu. Wakati dhambi zetu za zamani zinakuja akilini, tunaweza kuchagua kuzitilia maanani (kwa sababu hio tunapata kuwa na hisia za hatia), au tunaweza kuchagua kujaza mawazo yetu na mawazo ya Mungu mwenye kushangaza ambaye alitusamehe na kumshukuru na kumsifu(Wafilipii 4: 8) Kukumbuka dhambi zetu ni manufaa tu wakati inatukumbusha kiwango cha msamaha wa Mungu na inafanya iwe rahisi zaidi kusamehe wengine (Mathayo 18: 21-35).
Kwa kusikitisha, kuna watu ambao "hawajisamehe wenyewe," yaani, ambao hawasongi mbele zaidi, kwa sababu hawataki kusahau dhambi zao za zamani. Wengine huchagua kuendelea kupata furaha kubwa kutokana na dhambi za zamani walizozingatia katika akili zao. Hili, pia, ni dhambi na lazima lmtu akiri na kuasi dhambi hio. Mtu anayetamani mwanamke moyoni mwake ana hatia ya dhambi ya uzinzi (Mathayo 5:28). Kwa njia ile ile, kila wakati tunapofikiria dhambi zetu, tunafanya dhambi hiyo tena. Ikiwa haya yanafanyika katika maisha ya Mkristo, ule mtindo wa dhambi / hatia / dhambi / hatia unaweza kuwa na uharibifu usio na mwisho.
Tunapokumbuka kwamba dhambi zetu zimesamehewa inakua rahisi kuwasamehe wengine dhambi zao (Mathayo 7: 1-5; 1 Timotheo 1:15). Msamaha unapaswa kutukumbusha juu ya Mwokozi mkuu ambaye alitusamehe, ingawa hatukustahili kamwe, na tunapaswa kukaribia Kristo kwa kumtii kwa upendo (Warumi 5:10; Zaburi 103: 2-3, 10-14). Mungu ataruhusu dhambi yetu kuja katika akili (Shetani anaweza kuitaka iwe kwa madhumuni mabaya, lakini Mungu anairuhusu kwa kusudi nzuri), lakini anataka tukubali msamaha Wake na kufurahia neema yake. Kwa hivyo, wakati unakumbuka dhambi zako za zamanil, "kubadilisha nia" kwa kuchagua kutegemea huruma zake (inaweza kusaidia kufanya orodha ya mistari ya Biblia ambayo inakuhimiza kusifu) na kufikiria jinsi tunapaswa kuchukia dhambi.
English
Biblia inasema nini kuhusu kujisamehe mwenyewe?