settings icon
share icon
Swali

Je! Ninawezaje kujua kama nimeitwa kuwa mhubiri?

Jibu


Hamna shaka kuwa kuhubiri ni wito mzuri na ambao ni muhimu kwa Mungu (1 Timotheo 3: 1-7; Yakobo 3: 1; Waefeso 4: 11-16). Kuhubiri sio tendo la kuziba muda katika ibada, wala sio kushiriki uzoefu wa kibinafsi, haijalishi ni wa kusisimua namna gani kihisia. Wala sio "mazungumzo" yaliyopangwa vizuri ili kutoa hatua ziongozao kwa maisha bora. Kuhubiri, kama vile mtume Paulo anavyoandika, ni chombo kama gari ambacho kwayo ukweli wa injili ya uzima ya Yesu Kristo unawasilishwa. Maneno ya mhubiri yanapaswa kuwa aminifu kwa Neno la Mungu, ambalo ni "uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye" (Warumi 1:16). Himizo la Paulo kwa mchungaji mchanga Timotheo linasisitiza kuweka kazi ya kuhubiri mbele kwanza: "Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu. . . Hubiri Neno; kuwa tayari" (2 Timotheo 4: 1-2). Kwa hivyo hamna shaka kuwa kulihubiri Neno ni muhimu sana kwa Mungu. Mtu yeyote anayefikiria kuingia kwenye huduma kama mhubiri anapaswa pia kuliona Neno la Mungu kama la kipaumbele cha kwanza.

Lakini, je! mtu anawezaje kuwa na uhakikisho kuwa ameitwa kuwa mhubiri? Kwanza viashirio nyenyekevu. Ikiwa mtu ana haja sana ndani yake ya kuhubiri-nia ambayo haiwezi kataliwa-hicho ni kielelezo bora cha "wito" wa Mungu. Mtume Paulo na Yeremia nabii wa Agano la Kale walikuwa na haja hiyo ya kulitangaza neno la Mungu. Paulo alisema, "Lakini ninapohubiri Injili siwezi kujisifu maana ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipoihubiri Injili! (1 Wakorintho 9:16). "Kulazimika" kuhubiri injili inamaanisha kuwa na msukumo wa ndani na lazimisho lisiloepukika na kukataliwa ili kufanya hivyo. Yeremia alielezea msukumo huu kama "moto unaowaka" (Yeremia 20:8-9) ambao hauwezi kuzimwa. Kujaribu kulizuia ilimfanya kuwa mchovu sana.

Pili ni viashiria vya lengo la wito wa Mungu kuhubiri. Ikiwa mwitikio wa juhudi za kwanza katika kuhubiri ni mzuri, hii ni dalili nzuri kwamba mhubiri mtarajiwa ana karama ya didaktikos, ambayo ni karama ya kufundisha, kutoka kwa Roho Mtakatifu (Waefeso 4:11). Kila mhubiri kwanza lazima awe mwalimu wa Neno la Mungu, akiwasilisha kwa ufasaha na kwa muhtasari na kuliwe njia wasilizaji wataweza kuliweka katika matendo kibinafsi. Viongozi wa kanisa kwa kawaida ndio waamuzi bora wa ikiwa mtu fulani ana karama hii. Ikiwa wamekubaliwa kuwa ana karama hiyo, mhubiri huyo mtarajiwa lazima achunguzwe na uongozi kuhusu tabia yake, kama ilivyoainishwa katika mahitaji ya wazee katika 1 Timotheo 3 na Tito 1. Uthibitisho huu mara mbili, kanisa ni dalili nyingine ya wito wa Mungu.

Mwishowe, kila hatua moja baada ya nyingine ya mchakato wote unapaswa kufanywa kwa maombi. Ikiwa kweli Mungu anamwita mtu kuhubiri, atathibitisha kwa njia nyingi. Ikiwa unahisi unaitwa kuhubiri, tafuta uso wa Mungu na umwombe fursa zaidi na uthibitisho zaidi wa ndani na wa nje. Pia muuliza aifanya dhihirisha ikiwa sio mapenzi yake kuendelea. Jipe moyo kwa ukweli kwamba Mungu ndiye mfalme na anaongoza vitu vyote na atafanya kazi "katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake" (Warumi 8:28). Ikiwa amekuita kuhubiri, wito huo hauwezi kukataliwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ninawezaje kujua kama nimeitwa kuwa mhubiri?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries