Je! Makosa kwa wanandoa kuishi pamoja kabla ya ndoa?


Swali: "Je! Makosa kwa wanandoa kuishi pamoja kabla ya ndoa?"

Jibu:
Jibu kwa swali hili linategemea hasa ni nini inamaanishwa kwa “kuishi pamoja.” Kama inamaanisha kuwa na tendo la ndoa, basi hapo ni mbaya. Ngono kabla ya ndoa imekashifiwa mara nyingi sana katika maandiko, pamoja na aina zingine za usherati (Matendo Ya Mitume 15:20; Warumi 1:29; 1 Wakorintho 5:1; 6:13, 18; 7:2; 10:8; 2 Wakorintho 12:21; Wagalatia 5:9; Waefeso 5:3; Wakolosai 3:5;1 Wathesalonike 4:3; Yuda 7). Bibilia inapendekeza kinyuea ngono nche ndoa hadi wakati wa ndoa. Ngono kabla ya ndoa ni mbay vile uzinzi ulivyo mbaya na aina zingine za usherati, kwa sababu zote zausika na mtu ambaye hamjaoana naye kihalali.

Kama “kuishi pamoja” inamaanisha kukaa katika nyumba moja, basi hilo ni jambo lingine tofauti. Hasa hamna ubaya wowote kati ya mume na mke wakikaa kwa nyumba moja kama hakuna usherati wowote unaofanyika. Ingawa, shida inayojibuka ni, kule kuonekana kwa ile dhamira ya usherati (1 Wathesalonike 5:22; Waefeso 5:3), na litakuwa jaribio kubwa sana kwa usherati (1 Wakorintho 6:18). Pia kuna ile dhamira ya usherati. Wachumba wanao kaa pamoja inachukuliwa kuwa wanalala pamoja hiyo ndio hali ya mambo. Hata kama kukaa katika nyumba moja sio dhambi bali kuna ile picha ya dhambi inayoonekana. Bibilia inatuambia tuiepuke hiyo dhamira ya dhambi (1 Wathesalonike 5:22; Waefeso 5:3), kuutoroka usherati, na tusimfanye yeyote akwasike au akasirishwe. Kwa sababu hiyo, haimuheshimu Mungu kwa mume na mke kukaa pamoja nche ya ndoa.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Makosa kwa wanandoa kuishi pamoja kabla ya ndoa?

Jua jinsi ya ...

kutumia milele na MunguPata msamaha kutoka kwa Mungu