settings icon
share icon
Swali

Je! Tunaishi katika nyakati za mwisho?

Jibu


Biblia inasema unabii wa matukio mengi ambayo yatatokea katika nyakati za mwisho. Matukio haya yanaweza kuhesabiwa kama ishara za asili, ishara za kiroho, ishara ya kijamii, ishara za kiteknolojia, na dalili za kisiasa. Tunaweza kuangalia kile ambacho Biblia inasema juu ya mambo haya, na, kama ishara zipo katika wingi, tunaweza kuwa na uhakika kwamba sisi, kwa kweli, tunaishi katika nyakati za mwisho.

Luka 21:11 huorodhesha baadhi ya ishara za asili ambazo zitatokea kabla ya kuja kwa pili kwa Yesu: "Kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni." Wakati hatupaswi kutafsiri kila maafa ya asili kama ishara ya nyakati za mwisho, kuongezeka kwa majanga ya asili inaonekana kuwa tunajitayarisha kwa kile kinachokuja- "uchungu wa uzazi," kama Yesu alivyouita (Mathayo 24: 8).

Biblia inataja ishara zenye nguvu na mbaya za kiroho. Katika 2 Timotheo 4: 3-4 tunatambua kwamba watu wengi watafuata walimu wa uongo. Sasa tunaona ongezeko la makundi ya kitamaduni, ukatili, udanganyifu, na uchawi, na wengi wanachagua kufuata kizazi kipya au dini za kipagani. Kwa uzuri, Yoeli 2: 28-29 anatabiri kwamba kutakuwa na uchafu mkubwa wa Roho Mtakatifu. Unabii wa Yoeli ulitimizwa siku ya Pentekoste (Matendo 2:16), na bado tunaona matokeo ya ujazo huo war oho katika uamsho na harakati za Wakristo zinazoongozwa na Roho, na katika kuhubiri ujumbe wa injili duniani kote.

Pamoja na ishara katika maeneo ya asili na ya kiroho, kuna ishara katika jamii. Uovu unaoenea katika jamii hii leo ni dalili ya uasi wa wanadamu dhidi ya Mungu. Uaviaji mimba, ushoga, matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na unyanyasaji wa watoto ni ushahidi kwamba "wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu" (2 Timotheo 3:13). Sasa tunaishi katika jamii ya anasa na wapenda fedha. Watu wanajipenda wenyewe- "kutafuta kuwa wa kwanza" na kufanya mambo yanayo onekana ni ya haki machoni pao wenyewe. Mambo yote haya, na mengine mengi, yanaweza kuonekana karibu na sisi kila siku (angalia 2 Timotheo 3: 1-4).

Utekelezaji wa unabii wa nyakati za mwisho ulionekana kuwa haiwezekani mpaka ujio wa teknolojia ya kisasa. Baadhi ya hukumu katika Ufunuo ni rahisi zaidi kufikiria katika umri wa nyuklia. Katika Ufunuo 13, Mpinga Kristo anasemekana kudhibiti biashara kwa kulazimisha watu kuchukua alama ya mnyama, na, kutokana na maendeleo ya kisasa ya teknolojia ya tarakilishi, zana ambazo atazitumia zinaweza kuwa hapa tayari. Na kwa njia ya mtandao, redio na televisheni, injili inaweza sasa kutangazwa kwa ulimwengu wote (Marko 13:10).

Na kuna dalili za kisiasa. Kurejeshwa kwa Israeli kwa nchi yake mwaka wa 1948 ni unabii mmoja unaovutia sana ambao unathibitisha kuwa tunaishi katika nyakati za mwisho. Wakati wa karne ya 20, hakuna mtu angeweza kuwa na ndoto ya kwamba Israeli angekuja tena katika nchi yake, achana ni kuimiliki Yerusalemu. Yerusalemu ni dhahiri iko katikati mwa siasa na inasimama peke yake dhidi ya maadui wengi; Zakaria 12: 3 inathibitisha hivi: "Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake." Mathayo 24: 6-7 alitabiri kwamba" taifa litaamka juu ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. "" Vita na uvumi wa vita " Dhahiri ni dalili ya wakati huu wa sasa.

Hizi ni ishara chache tu ambazo zinaonyesha kwamba tunaishi nyakati za mwisho. Kuna nyingi zaidi. Mungu alitupa unabii huu kwa sababu hataki mtu yeyote apotee, na Yeye hutoa onyo mara nyingi kabla ya kumwaga ghadhabu Yake (2 Petro 3: 9).

Je! Tunaishi katika nyakati za mwisho? Hakuna mtu anayejua wakati Yesu atarudi, lakini unyakuzi unaweza kutokea wakati wowote. Mungu ataadhibu dhambi kupitia kwa neema au kwa ghadhabu. Yohana 3:36 inasema, "Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia." Wale ambao hawakubali Yesu Kristo kama mwokozi wao wataendelea chini ya ghadhabu ya Bwana.

Habari njema ni kwamba hatuchachelewa sana kuchagua uzima wa milele. Yote ambayo inahitajika ni kukubali kwa imani zawadi ya Mungu ya neema ya bure. Hakuna kitu unaweza kufanya ili upate neema; Yesu amelipa gharama kwa niapa yako (Warumi 3:24). Je! Uko tayari kwa kurudi kwa Bwana? Au utapatana na ghadhabu yake?

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunaishi katika nyakati za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries