settings icon
share icon
Swali

Nita ishi maisha yangu kwa ajili ya Mungu vipi?

Jibu


Mungu ametupa maelekezo ya wazi sana katika Neno Lake kuhusu jinsi tutakavyoishi kwa ajili yake. Hizi ni pamoja na amri ya kupendana (Yohana 13: 34-35), wito wa kumfuata kwa gharama ya kukataa tamaa zetu wenyewe (Mathayo 16:24), kuhimiza kutunza maskini na wahitaji (Yakobo 1: 27), na onyo la kutoingia katika tabia za dhambi, kama wale wasiomjua Mungu (1 Wathesalonike 5: 6-8). Yesu alielezea maisha yaliyoishi kwa ajili Mungu wakati mwalimu wa sheria alimwuliza amri muhimu zaidi. Yesu akajibu, "Sikiliza, Ee Israeli, Bwana Mungu wetu,ni Bwana mmoja. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Ya pili ni hii: Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe. Hakuna amri kubwa kuliko hii "(Marko 12: 29-31).

Sala ya Yesu kabla ya kusulubiwa kwake pia inatia mwanga juu ya madhumuni yetu. Akizumgumzia waumini, aliomba, "Nimewapa utukufu ulionipa, wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja: Mimi ndani yao na wewe ndani yangu. Nao wawe na umoja kamili ili basi ulimwengu ujue kwamba umenituma na umewapenda kama vile umenipenda. Baba, nataka wale ambao umenipa kuwa pamoja nami pale nilipo, na kuona utukufu wangu, utukufu ambao umenipa kwa sababu umanipenda kabla ya uumbaji wa ulimwengu. Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nakujua na hao wemejua kwamba ndiwe uliyenituma. Nimekujulisha kwao, na itaendelea kuwajulisha ili upendo unao kwa ajili yangu uwe ndani yao na kwamba mimi mwenyewe niwe ndani yao "(Yohana 17: 22-26). Yesu anatamani uhusiano nasi.

Katekisimu ya Westminster inasema, "Mwisho wa mtu ni kumtukuza Mungu, na kumfurahia milele." Maisha mtu anayoishi kwa ajili ya Mungu hutukuza Mungu. Tunamtafuta Mungu kwa moyo wetu wote — moyo, roho, akili, na nguvu. Tunakaa ndani ya Kristo (Yohana 15: 4, 8) na kwa hivyo tenda kama Yeye kwa kupenda wengine. Kwa kufanya hivyo, tunaleta utukufu kwa jina lake na pia kufurahia uhusiano ambao tuliumbiwa awali.

Wale wanaotaka kuishi kwa ajili ya Mungu lazima wamtafute katika Neno Lake. Tunapaswa kutafuta uongozi wa Roho Mtakatifu ili kulitumia Neno kwa maisha yetu. Kuishi kwa ajili ya Mungu inamaanisha kujitoa na kutamani mapenzi ya Mungu kuliko yote. Tunapomkaribia Mungu na kumjua zaidi, tamaa zake zitakuwa kawaida zetu. Tunapokomaa, tamaa yetu ya kutii amri za Mungu inakua jinsi upendo wetu kwake unaongezeka. Kama Yesu alivyosema, "Ikiwa unanipenda, utasikiliza ninayoamuru" (Yohana 14:15).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nita ishi maisha yangu kwa ajili ya Mungu vipi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries