settings icon
share icon
Swali

Kwa nini kuhesabiwa haki kwa imani ni mafundisho muhimu sana?

Jibu


Mafundisho ya kuhesabiwa haki kwa imani yanatenganisha Ukristo wa kibiblia kutoka kwa mifumo yote ya imani. Katika kila dini, na katika baadhi ya vietengo vya kile kinachoitwa "Ukristo," mtu anafanya njia yake kwa Mungu. Ni katika Ukristo wa kibiblia amabapo mtu anaokolewa kwa neema kupitia imani. Tunaporejelea kwa Biblia tunaona kwamba kuhesabiwa haki ni kwa imani,sio kwa matendo.

Kuhesabika haki inamaanisha "kutamkwa au kufanya kama mwenye haki." Kwa Mkristo, kuhesabiwa haki ni tendo la Mungu sio tu kusamehe dhambi za mwamini lakini kumtunukia haki ya Kristo. Bibilia inasema katika maeneo kadhaa kwamba kuhesabiwa haki ni kwa njia ya imani (kwa mfano, Warumi 5: 1; Wagalatia 3:24). Kuhesabiwa haki haukupatikani kupitia kazi yetu wenyewe; bali, tunafunikwa na haki ya Yesu Kristo (Waefeso 2: 8; Tito 3: 5). Mkristo, akihesabiwa kuwa mwenye haki, kwa hiyo amefunguliwa kutokana na hatia ya dhambi.

Kuhesabiwa haki ni kazi kamilifu ya Mungu, na niya mara moja, kinyume na utakaso, ambayo ni mchakato unaoendelea wa kukua ambao tunakuwa zaidi kama Kristo (kitendo cha "kuokolewa," tazama 1 Wakorintho 1:18; 1 Wathesalonike 5:23). Utakaso hutokea baada ya kuhesabiwa haki.

Kuelewa mafundisho ya kuhesabiwa haki ni muhimu kwa Mkristo. Kwanza, tunapoelewa tumehesabiwa haki na neema yake Mungu basi hio inasababisha kazi nzuri na ukuaji wa kiroho; Kwa hivyo, kuhesabiwa haki kunasababisha utakaso. Pia, ukweli kwamba kuhesabiwa haki ni kazi ya Mungu iliyokamilika inamaanisha kwamba Wakristo wana uhakika wa wokovu wao. Mbele ya macho ya Mungu, waumini wana haki inayofaa ili kupata uzima wa milele.

Mara tu mtu anapohesabiwa haki, hakuna kitu kingine anachohitaji ili apate kuingia mbinguni. Kwa kuwa kuhesabiwa haki ni kwa kupitia imani katika Kristo, kulingana na kazi Yake kwa niaba yetu, kazi zetu wenyewe hazistahiki kama njia ya wokovu (Warumi 3:28). Kuna mifumo mikubwa ya kidini yenye teolojia nyingi zinazofundisha mafundisho ya uwongo ya kuhesabiwa haki kwa matendo. Lakini wanafundisha "injili tofauti-ambayo sio injili ya kweli" (Wagalatia 1: 6-7).

Bila ufahamu wa kuhesabiwa haki kwa imani peke yake, hatuwezi kutambua kweli zawadi ya utukufu — "neema tusiyoistahili" ya Mungu inakuwa "yenye sifa" katika akili zetu, na tunaanza kufikiri tunastahili wokovu. Mafundisho ya kuhesabiwa haki kwa imani inatusaidia kudumisha "kujisalimisha kwa Kristo" (2 Wakorintho 11: 3). Kuamini kuhesabiwa haki kwa imani kunatuzuia kudanganyika kwamba tunaweza kuingia mbinguni kupitia matendo tu. Hakuna ibada, hakuna sakramenti, hakuna kazi ambayo inaweza kutufanya tustahili utakatifu wa Kristo. Ni kwa neema yake tu, kwa kulingana na imani yetu, kwamba Mungu alitupa utakatifu wa Mwanawe. Wala Agano la Kale na Agano Jipya inasema, "Waadilifu wataishi kwa imani" (Habakuki 2: 4; Warumi 1:17; Wagalatia 3:11; Waebrania 10:38).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini kuhesabiwa haki kwa imani ni mafundisho muhimu sana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries