settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya kuharimisha katika Biblia?

Jibu


Kwanza, tunapaswa kutambua kwamba Biblia haitumii neno kuharimisha/kutengwa. Ni neno ambalo limekubaliwa na vikundi kadhaa vya kidini, haswa Kanisa la Katoliki, kuashiria mchakato rasmi wa kumwondoa mtu kutoka uanachama na kushiriki kanisani, kutoka kwa uhusiano na jamii ya kanisa, au, kwa maoni ya Katoliki, hata kutoka kwa familia ya Mungu.

Ingawa Biblia haifundishi kwamba Mkristo anaweza kupoteza wokovu wake, lakini inaelezea mchakato wa nidhamu ya kanisa katika vifungu kadhaa. Hatua ya mwisho ya nidhamu ya kanisa ni kutengwa na kanisa — kuondolewa kutoka kwa kanisa lako la ushirika.

Katika Mathayo 18: 15-17, Yesu anawafundisha wanafunzi Wake juu ya kumwondoa mtu kutoka kwa kanisa. Bwana anaelezea njia kadhaa za kuitikia makosa ya dhambi katika jamii ya kanisa:

Hatua ya 1: Mwendee mtu huyo kwa siri, mwambi vile amekukosea, na mpatane ikiwa akao tayari. Ikiwa mtu aliyekukosea atatubu, hakuna hatua nyingine inayohitajika.

Hatua ya 2: Ikiwa hatasikiza, mrudie na mashahidi wawili au watatu ili mfanye mazungumzo tena, kudhibitisha ukweli na ushahidi.

Hatua ya 3: Ikiwa bado anakataa kusikiza na kutubu kutoka kwa dhambi yake, mlete mbele ya kanisa nzima na ufanye uamuzi dhidi yake.

Hatua ya 4: Ikiwa bado hatubu, kanisa linapaswa kumtenga mtenda dhambi huyo. Maneno ya Yesu ni "basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru" (Mathayo 18:17, NEN).

Wayahudi waliona vikundi vyote viwili ambavyo Yesu anavitaja — watu wa mataifa na watoza ushuru — kama watu wasio amini. Mataifa walikuwa makafiri waabudu sanamu, na watoza ushuru walikuwa wakishirikiana na Roma. Katika siku za Yesu, Waisraeli wana dini hawangeshirikiana zaidi ya kile kilichokuwa ni cha watu wa mataifa au watoza ushuru. Hawangekula chakula pamoja nao, au kuwaalika kwenye mikusanyiko yao ya kijamii. Kwa hivyo, wakati Yesu anasema kuwa tuwaone wenye dhambi wasiotubu kanisani kama "Mtu wa asiyeamini na mtoza ushuru," Yeye analiagiza kanisa kuacha rasmi na kwa mawasiliano ya wazi likomeshe kuwa na ushirika wa karibu na mwenye dhambi ambaye hajatubu; mtenda dhambi anapaswa kuwekwa mbali na jamii ya Wakristo. Hii ni kutengwa/kuharimishwa.

Je! kusudi la kutengwa ni gani? Kufukuzwa kwa mwenye dhambi asiyetubu, aliyekataa kutoka kwa jamii ya waumini sio juu ya kumwaibisha hadharani au kumhukumu. Ni juu ya kumpenda mtu huyo vya kutosha kufanya kile kinachomfaa yeye na kufanya kile kilicho bora kwa kanisa lote kwa ujumla.

Tunayo mfano wa kutengwa na matokeo yake katika vifungu viwili kutoka kwa Paulo. Mwanamume mmoja katika kanisa la Korintho alikuwa anafanya uzinzi na mamake wa kambo, dhambi mbaya sana "hata miongoni mwa watu wasiomjua Mungu" (1 Wakorintho 5: 1). Paulo anawakemea Wakristo huko Korintho kwa kukubali kujamihana kwa maharimu huyo. Vile inavyoonekana, Wakorintho walikuwa wameelewa vibaya neema ya Mungu vibaya sana kiwango kwamba waliamini kuwa dhambi zote zinapaswa kuvumiliwa, labda hata kusherehekewa bila haya, kama ushahidi wa neema na msamaha wa Mungu (aya ya 2).

Paulo anasema, "Haiwapaswi." Dhambi kanisani lazima iadhibiwe. Anawaamuru Wakorintho kukusanyika pamoja kwa kusudi la kuharimisha mtu kutoka kanisa. Kanisa la waumini wa eneo hilo, chini ya mamlaka ya kitume, wanafaa kumkabidhi mtu huyu kwa Shetani kwa "ili mwili wake uharibiwe, ili roho yake iokolewe katika siku ya Bwana" (1 Wakorintho 5: 4-5). Ni dhahiri, katika kesi hii, kulikuwa na kuadhirika kimwili kusio kwa kawaida ambako kunahusishwa na kutengwa kutoka kwa kanisa; ilikuwa kutengwa na kuongezea laana ya kitume.

Maandiko hayaonyeshi kuwa kila kutengwa kunafuatwa na athari za mwili. Kanuni ya jumla, hata hivyo, ni kwamba kutengwa kutoka kanisa humwezesha mwenye dhambi kupata matokeo mabaya, atharichungu za uchaguzi wake wa dhambi ili atubu, anyenyekee kwa Mungu, na aokolewe na uharibifu wa kiroho. Sababu ya kutengwa sio adhabu au kulipisa kisasi bali ni mageuzo na afya ya kiroho.

Barua ya pili ya Paulo kwa Wakorintho inashughulikia kumfuatilia mtu huyo baada ya kumtenga kutoka kanisa. Katika 2 Wakorintho 2: 5–11, Paulo anaonekana kuzungumzia juu ya mtu yuyo huyo ambaye alikuwa ameamuru kanisa imtenge. Mtenda dhambi alikuwa ametubu, na Paulo anaandika, "Adhabu hii aliyopewa na wengi inamtosha. Basi sasa badala yake, inawapasa kumsamehe na kumfariji, ili asigubikwe na huzuni kupita kiasi. Kwa hiyo, nawasihi, mpate kuuthibitisha tena upendo wenu kwa ajili yake" (aya ya 6-8). Pindi tu huyu muumini aliyetengwa ametubu, anapaswa kukaribishwa tena katika uhusiano mzuri na jamii ya kanisa. Pindi toba imethibitishwa, kutengwa kutoka kwa kanisa kunapaswa kuachwa kibisa. Lengo limetimizwa.

Kwa hivyo, ni nani anayefaa kutengwa? Bibilia ii wazi kuwa kutengwa kunafaa kufanywa na washirika wa kanisa tu (sio wale wasioamini) na ni kwa mjibu wa dhambi dhahiri na inayoendelea ambayo kwayo mtu amekataa kutubu licha ya maonyo mengi: "Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye" (1 Wakorintho 5:11).

Mambo tano muhimu ya kukumbuka juu ya kumtengwa mtu kutoka kwa kanisa:

1. Biblia kamwe haiagizi Wakristo binafsi kuamua peke yao au hata katika kikundi kidogo "kumtenga" miimini mwingine. Kutengwa kunanuiwa kuwa hatua rasmi inayochukuliwa na kanisa kwa ujumla.

2. Kutengwa ni hasa ni juu ya uhusiano. Wale walio kanisani wameagizwa haswa kuacha kushiriki chakula na mtu asiyetubu (1 Wakorintho 5:11), kupunguza mawasiliano yao naye.

3. Mchakato huu wa kutengwa na waumini ni jukumu la waumini, kwa wale wanaojitangaza kuwa wamemwamini Kristo kwa dhati kwa wokovu wao. Kutengwa ni itikio la kanisa kwa yule anayesema, "Naam, mimi ni Mkristo, na, la, sitageuka kutoka dhambi hii."

4. Mchakato wa kutengwa haunuiwi kuwa wa mtu ambaye anakubali dhambi yake na ametubu lakini anaendelea kujaribiwa kutika kuachana nayo. Ikiwa muumini atatenda dhambi na, wakati anapokabiliwa, aseme, "Naam, hiyo ilikuwa makosa. Samahani. Nataka kuanza upya tena," atasamehewa — hata ikiwa ametenda dhambi hiyo hiyo mara nyingi (Mathayo 18: 21–22). Katika hali kama hiyo, Maandiko hayashauri kwamba dhambi ya mtu huyo inapaswa kuelezewa kanisa kama aina ya adhabu, isipokuwa yeye mwenyewe aamue kuitangaza.

5. Lengo la kutengwa ni urejesho. Kulingana na Yesu, mchakato wote wa kumuondoa mshirika kanisani unapaswa kuwa wa hatua kwa huta, wa makusudi, na kwa uangalifu. Ikiwa katika wakati wowote wa mchakato mtu aliyetenda dhambi atubu, basi "utakuwa umempata tena ndugu yako" (Mathayo 18:15), na ushirika huo utarejeshwa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya kuharimisha katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries