settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kufungwa nira isiyo na usawa?

Jibu


Maneno " kufungwa nira isiyo na usawa" yanajitokeza katika 2 Wakorintho 6:14: "Msifungwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana kuna ushirika gani kati ya haki na uasi? Tena pana ushirika gani kati ya nuru na giza? "Toleo jingine linasema," Usifungane pamoja na wasioamini. "

Juku au nira ni ile mbao ambayo inaunganisha ng'ombe wawili kwa kila mmoja na kwa mzigo wao wanaovuta. Timu "iliyofungwa nira isiyo na usawa" ina ng'ombe mmoja mwenye nguvu na mmoja mwenye udhaifu, au mrefu zaidi na moja mfupi. Yule mdhaifu au mfupi anaweza kutembea polepole kuliko yule mrefu, mwenye nguvu, na kusababisha mzigo kuzunguka kwenye miduara. Wakati ng'ombe wanapofungwa nira isiyo na usawa, hawawezi kufanya kazi iliyowekwa mbele yao. Badala ya kufanya kazi pamoja, wao hufanya kazi kinyume na mwingine.

Ushauri wa Paulo katika 2 Wakorintho 6:14 ni sehemu ya hotuba kubwa kwa kanisa la Korintho juu ya maisha ya Kikristo. Aliwazuia wasiwe na ushirikiano usio sawa na wasioamini kwa sababu waumini na wasioamini ni kinyume, kama vile vile mwanga na giza. Hawana kitu sawa, kama vile Kristo hana kitu sawa na "Belia" (Belial) neno la Kiebrania linalomaanisha "kutokuwa na maana" (mstari wa 15). Hapa Paulo hutumia neon hili kumaanisha shetani. Dhana hii ni kwamba ulimwengu wa kipagani, uovu, usioamini, unaongozwa na kanuni za Shetani, na kwamba Wakristo wanapaswa kuwa tofauti na ulimwengu mwovu, kama Kristo alivyojitenga na njia zote, makusudi, na mipango ya Shetani. Hakuwa na ushirikisha nao, Yeye hakuunda muungano pamoja nao, na ni lazima iwe vivyo hivyo kwa wafuasi wa wa Kristo. Kujaribu kuishi maisha ya Kikristo na mtu asio Mkristo kama rafiki yetu wa karibu na mshiriki kutatufanya tuzunguke kwenye miduara.

"Nira isiyo sawa" mara nyingi hutumiwa kwa mahusiano ya kibiashara. Kwa Mkristo kuingia katika ushirikiano na mtu asiyeamini ni kama kualika mabaya. Wana maoni yanayopinga ya ulimwengu na maadili. Maamuzi ya biashara ambayo yanapaswa kufanywa kila siku husema mengi kuhusu moja au mwingine. Kwa uhusiano wao kufanya kazi, mmoja au yule mwingine lazima kuacha maadili yake na kuhamia kuelekea kwa maadili ya yule mwingine. Mara nyingi zaidi , ni mwamini ambaye anajikuta akilazimishwa kuwacha kanuni zake za Kikristo nyuma kwa ajili ya faida na ukuaji wa biashara.

Bila shaka, uhusiano wa karibu sana mtu mmoja anaoweza kuwa nao ni uhusioano wa ndoa, na hivi ndivyo jinsi kifungu hiki kinatafsiriwa. Mpango wa Mungu ni kwa mwanamume na mwanamke kuwa "mwili mmoja" (Mwanzo 2:24), uhusiano wa karibu sana kuwa moja kwa moja na kwa mfano anakuwa sehemu ya mwingine. Kuunganisha mwamini na asiyeamini niu kuunganisha wasio na usawa au wanaotofautiana, ambayo inafanya uhusiano kuwa mgumu sana.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kufungwa nira isiyo na usawa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries