Swali
Bibilia inasema nini kuhusu kufunga kwa Wakristo?
Jibu
Maandiko hayamshurutishi Mkristo kufunga. Mungu haitaji au kuamuru Wakristo wafunge. Kwa wakati huo huo, Bibilia inawazilisha kufunga kama kitu ambacho ni kizuri, cha muimu na cha manufaa. Kitabu cha Matendo Ya Mitume kimerekodi kuwa Wakristo walifunga kabla ya kufanya uamuzi wa maana (Matendo Ya Mitume 13:2, 14:23). Kufunga na maombi kila mara zimeambatanishwa pamoja (Luka 2:37; 5:33). Kila mara, angazo la kufunga ni kutokuwa na chakula. Badala ya lengo kuwa, kufunga ni kuyapeleka mawazo yako nche ya vitu vya dunia na kiukamilifu kumtazamia Mungu. Kufunga ni njia mojawapo ya kudhihirishia Mungu na sisi wenyewe kwamba hatutaki mchezo katika uhusiano wetu na yeye. Kufunga kunatuzaidia kupata mtazamo na kufanya upya tegemeo letu kwa Mungu.
Ingawa kufunga katika maandiko karibu kila mara ni kufunga kutoka chakula, kunazo njia nyingine za kufunga. Kitu chochote kimeachwa kwa muda ili kuweka mawazo yetu kwa Mungu chaweza chukuliwa kufunga (1 Wakorintho 7:1-5). Kufunga lazima kuwe na mipaka muda uwekwe hasa wakati tunafunga kutoka kwa chakula. Muda ulioongezwa bila kukula unaweza kuwa wa madhara kwa mwili. Kufunga hakuko kwa madhumuni ya kuuteza mwili, bali kuyaelekeza mawazo yetu kwa Mungu. Kufunga kusichukuliwe kuwa “ratiba ya chakula.” Lengo la kibibilia la kufunga sio kupunguza uzito, bali kupata ushirika wa ndani na Mungu. Mtu yeyote anaweza kufunga, lakini wengine huenda hawataweza kufunga kutoka kwa chakula (Wenye ugonjwa wa sukari). Kila mtu anaweza anaweza kuacha kitu chochote kwa muda na kuleta mawazo yake karibu na Mungu.
Kwa kuchukua macho mbali na vitu vya dunia, tunaweza zaidi kuyaweka mawazo yetu kwa Kristo. Kufunga sio njia ya kumfanya Mungu atende vile tunavyotaka. Kufunga kunatubadilisha, sio kumbadilisha Mungu. Kufunga sio njia ya kuonekana mwokovu sana kuliko wengine. Kufunga kunastahili kufanyika kwa moyo wa unyenyekevu na nia ya furaha. Mathayo 6:16-18 yasema, “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamna; maana hujiimbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
English
Bibilia inasema nini kuhusu kufunga kwa Wakristo?