settings icon
share icon
Swali

Kuna maana gani ya wale waliofufuliwa katika kifo cha yesu (Mathayo 27:52-53)?

Jibu


Mathayo 27:50-53 imerekodi, "Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho. Hapo pazia la hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunguliwa; nao baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika nji mtakatifu wakaonekana na watu wengi."

Tukio hili lilifanyika kama ushuhuda kwa nguvu za milele zilizopewa Yesu Kristo pekee (1Timotheo 6:14-16). Ni Mungu pekee ana nguvu ya maisha na kifo (1Samueli 2:6; Kumbukumbu 32:29). Kwa hivyo, ufufuo ndio nguzo kuu ya Ukristo. Dini zingine zote na viongozi wao hawamtumikii Kristo aliyefufuka. Kwa kushinda kifo, Yesu Kristo papo hapo alipokea heshima za ziada kwa sababu alifufuka huku kila mfu alizalia kabruni. Ufufuo umetupa sababu ya kuwajulisha wengine kuhusu Yeye na kuweka imani kwa Mungu (1Wakorintho 15:17). Paulo anasema wazi katika ayah ii kuwa hakuna ufufuo unaolinganishwa na msamaha wa bure wa dhambi zetu. Na mwishoye, ufufuo umetupa sababu ya kuwa na tumaini leo hii (1 Wakorintho 15:20-28). Ikiwa Kristo hakufufuliwa toka kwa wafu, basi Wakristo hawangekuwa salama kiroho kuliko wenye sio wakristo. But ukweli ni kwamba Mungu alimfufua "Bwana wetu Yesu, kutoka kwa wafu. Yeye alitolewa auawe kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka ili tufanywe waadilifu" (Warumi 4:24-25).

Ufufuo wa watakatifu unaingiana sana na ufasaha na mikakati iliyotumika na Mathayo katika Injili yake. Chunguza Ezekieli 37 na mifupa iliyopewa uhai pamoja na hadhiti hii unafunua kuwa unabii wa Agano la Kale ulitimilika katika ufufuo wa watakatifu. Kwa kuongezea, ufufuo wa watakatifu unahusiana moja kwa moja na ufalme unaokuja. Kufufuliwa kwa baadhi ya watakatifu na sio wote kunaonyesha kwamba Yesu ana nguvu za kufufua, lakini pia inatuelekeza katika ujio wa pili na hukumu ya Yesu Kristo, ambazo zitajumlisha wale wote ambao majina yao kwa imani na katika neema ya Mungu yameandikwa katika Kitabu cha Uzima. Kujua kwamba Yesu amekufa na kushinda mauti kupitia ufufuo wake unapaswa kuharakisha nia zetu za kutubu na kumwamini Yeye pekee kwa wokovu ili na sisi siku moja tufufuliwe "kwa kufumba na kufumbua" (1 Wakorintho 15:52).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuna maana gani ya wale waliofufuliwa katika kifo cha yesu (Mathayo 27:52-53)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries