settings icon
share icon
Swali

Je! Mkristo anafaa kutangaza kufilisika kwake?

Jibu


Ijapokuwa Biblia haisungumzii kufilisika kwa uhalisi, tuna kanuni ambazo zinaweza kutumika na kwa hiyo zitatusaidia kufanya uamuzi.

Kanuni ya Kibiblia # 1. Tuna jukumu la kuweka ahadi zetu na kulipa kile tunachopaswa. Mhubiri 5: 4-5 inasema, "Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri. Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe."

Kanuni ya Kibiblia # 2. Kuishi kwa mkopo na kukosa kulipa kile tunachodaiwa ni tabia ya waovu. Zaburi 37:21 inasema, "Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu." Wakristo hawapaswi kuwa na tabia kama ya "waovu."

Je, ni sahihi kwa Mkristo ambaye yu katika madeni kupata "zuluhisho la haraka" kwa tatizo lake kwa kutafuta kufilisika? Kulingana na aya hizi, jibu ni "Hapana." Mkristo ana wajibu wa kulipa kile alikubali kulipa, chini ya masharti ya awali ya makubaliano. Inaweza pelekea mabadiliko ya maisha na marekebisho makubwa ya bajeti, lakini uendeshaji mzuri wa fedha ni sehemu ya maisha ya kiungu.

Kuna baadhi ya aina za kufilisika ambazo zimepangwa kuahirisha ulipaji, badala ya kukimbia. Katika matukio hayo, madeni hayatafutwa, na kufungua moja kwa kufilisika kunatumia nia yake ya kulipa deni. Ulinzi wa mahakama hupanuliwa hadi mtu awe na uwezo wa kulipa. Aina hii ya kufilisika haiwezi kukiuka kanuni za Biblia zilizojadiliwa hapo juu na itakuwa, kwa Mkristo binafsi, itakua suala la dhamiri.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mkristo anafaa kutangaza kufilisika kwake?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries