settings icon
share icon
Swali

Tutafanya nini Mbinguni?

Jibu


Katika Luka 23:43, Yesu alisema, "Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi." Neno ambalo Yesu alitumia kwa "paradiso" ni paradeisos linamaanisha "Hifadhi, yaani, (hasa) Edeni (mahali pa furaha ya baadaye, paradiso)". Paradeisos ni neno la Kigiriki lililotolewa kwa neno la Kiebrania ambalo linamaanisha "Hifadhi: — msitu, bustani". Yesu alisema, "Leo utakuwa pamoja nami" en paradeisos, "si" en nephele "ambayo ni Kigiriki kwa" katika mawingu." Haja ni kwamba Yesu alliichukua na kulitumia neno kwa "bustani." Si tu bustani yoyote lakini "Paradiso ya Mungu" au Hifadhi ya Mungu (Ufunuo 2: 7) ambayo kwa ajili yetu itakuwa mahali pa furaha pa baadaye. Je, hapa panaonekana kama mahali pasipo na ucheshi? Wakati unafikiri juu ya Hifadhi, wafikiri juu ya mzononeko?

Yesu alisema, "Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake" (Mathayo 4:10). Ni kitu cha kuvutia kutambua kwamba Yesu hakusema "sifu na tumikia." Hata uchunguzi wa uepesi wa neno la sifa katika Biblia wa haraka unaonyesha kuwa ni maneno ya mdomo na ni sehemu kubwa ya kuimba. Kuabudu, hata hivyo, ni kutoka kwa moyo. Ibada inajidhihirisha katika sifa. Kumtumikia Mungu ni ibada, na Maandiko yako wazi tutamtumikia Mungu mbinguni. "Watumishi wake watamtumikia" (Ufunuo 22: 3).

Hatuwezi kumtumikia kikamilifu Mungu katika maisha haya kutokana na dhambi, lakini mbinguni "laana yote haitakuwa tena" (Ufunuo 22: 3). Hatutakuwa chini ya laana ya dhambi tena, hivyo kila kitu tukachofanya mbinguni itakuwa ibada. Hatuwezi kamwe kuhamasishwa na kitu chochote isipokuwa upendo wetu kwa Mungu. Kila kitu tukachofanya kitatokan na upendo wetu kwa Mungu, usio tiwa doha na asili yetu ya dhambi.

Basi tutafanya nini mbinguni? Jambo moja ni, tutajifunza. "Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?" (Waroma 11:34), "ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika" (Wakolosai 2: 3). Mungu ndiye "Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu" (Isaya 57:15). Mungu ni mkuu zaidi kuliko milele, na itachukua milele "ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo" (Waefeso 3: 18-19). Kwa maneno mengine, hatutaacha kujifundisha.

Neno la Mungu linasema hatutakuwa peponi Yake tu. "wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana" (1 Wakorintho 13:12). Hii inaonekana koaonyesha kwamba hatuwezi tu kujua marafiki zetu na familia pekee, bali tutawajua "kikamilifu". Kwa maneno mengine, hakuna haja ya siri mbinguni. Hakuna kitu cha kuwa na aibu. Hakuna kitu cha kujificha. Tutakuwa na milele kuingiliana na "mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha" (Ufunuo 7: 9). Hakuna ajabu mbinguni itakuwa mahali pa kujifunza kusio na mwisho. tutajua tu kila mtu ataishi milele!

Tarajio lolote zaidi juu ya kile tutafanya katika Hifadhi ya Mungu ya milele, mbinguni, itakuwa mbali zaidi wakati "Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu"(Mathayo 25:34). Chochote tutafanya, tunaweza kuwa na uhakika kuwa kitakuwa kizuri zaidi ya mawazo yetu!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tutafanya nini Mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries