settings icon
share icon
Swali

Nifanye nini ikiwa siwezi kuamua ni nani ninataka kumchumbia?

Jibu


Bibilia haizungumzii kwa makini mada hii, lakini inatupa ufafanuzi juu ya kile tunachopaswa kutafuta katika mwenzi wa ndoa. Ushauri wa kwanza, na bora, ni kuomba juu yake. Mungu atatoa hekima na mwongozo ikiwa utamwomba. "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa" (Yakobo 1: 5).

Wakorintho wa pili 6:14 hufundisha, "Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?" Swali la kwanza kuuliza ni kama atakaye kuwa mwenzi amejitolea kwa Mungu. Ikiwa hajajitolea, mtu huyo hapaswi kuzingatiwa kuwa mwenzi katika ndoa. Kwa upande mwingine, kwa sababu mtuo anafuata Kristo, hiyo haimfanyi kuwa chaguo bora. Kuwa "kutiwa nira pamoja" pia kunaweza kwenda zaidi ya "Je, yeye ni Mkristo?" Kuna imani nyingi tofauti katika Ukristo, na hii inapaswa kuzingatiwa wakati wa kuchagua mwanandoa mwenzi. Fikiria jinsi ndoa atakuwa ukiwa na mtu huyu. Je! Imani zenu zinakaribiana ya kutosha kwamba mnaweza kukubaliana kuwafundisha watoto wenu mafundisho hayo? Hili ni la umuhimu mkubwa.

Kwa wanaume, ni muhimu kuangalia ni nini mke Mkristo anapaswa kuwa. "Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo"(Waefeso 5: 22-24). Paulo anatuambia kwamba mke anapaswa kuwa chini ya mume wake, kwa upendo. Hii haimaanishi kwamba msichana unaofikiria kuwa na uhusiano naye anapaswa kujiwasilisha kabisa kwako. Katika kuchumbiana yeye halazimiki kufanya hivyo. Hata hivyo, yeye hapaswi kuwa na roho ya uasi, lakini anapaswa kujiwasilisha kwa mamlaka ako chini yake, kwa upendo. Anapaswa kuwa tayari kuongozwa. Methali 31: 10-31 inatuambia vile "mke wa tabia nzuri" anapaswa kuonekana. Yeye ni wa bidii, mwenye ukarimu na mwenye usaidizi, mwenye nguvu, na mwenye hekima. Huenda usipate sifa hizi zote kwa mtu mmoja, lakini hizi ni tabia nzuri na zinazompendeza Mungu.

Andiko lingine linaloelezea mke anayependeza Mungu ni 1 Petro 3: 1-4: "Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu." Hii inatuambia kwamba mwanamke anapaswa kuwa safi na kuishi kwa ajili ya Kristo ili apate kumrejesha mume aliye potea bil kutumia maneno yoyote. Pia inaonyesha kwamba hapaswi kuwa na wasiwasi juu ya vile anavyoonekana kwa nje bali vile anavyoonekana katika maisha yake ya kiroho.

Kwa wanawake, kuna mifano michache ya kile mume Mkristo anapaswa kuwa. Ingawa mtu unayemfikiria kuwa na uhusiano naye sio mume wako, unapaswa kuangalia sifa ambazo zinaonyesha aina hii ya upendo. "Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa" (Waefeso 5: 25-27). Je, yeye anajua kupenda? Je, yeye yu tayari kuwaongoza watu kuelekea Kristo na kuwasaidia wawe watakatifu na wasio na hatia? Je, ni kiongozi? Mwanamume anapaswa kumpenda Mungu kuliko kila kitu kingine na kuwa na nia ya kuwasaidia ndugu na dada zake katika Kristo kujitahidi kuwa watakatifu na kumpendeza Mungu. Anapaswa kuwa mnyenyekevu, mwenye hekima, na mwenye huruma, kama vile Kristo alikuwa. Tazama sifa hizi katika mwanaume, kwa sababu hii ndiyo inayompendeza Mungu.

Hutampata mtu "mkamilifu" aliye na sifa hizi zote, lakini Mungu atawawezesha kuona ikiwa mtu anamyefikiri kuwa na uhusiano naye anajitahidi kumpendeza Mungu. Kama ilivyo kwa uamuzi mwingine wowote katika maisha, mahusiano yanapaswa kuchukuliwa kwa busara, hekima, na kushughulikiwa kwa ufahamu na sala nyingi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nifanye nini ikiwa siwezi kuamua ni nani ninataka kumchumbia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries