settings icon
share icon
Swali

Nani anaruhusiwa kubatiza au kufanya ubatizo?

Jibu


Biblia haijaweka wazi jibu la swali hili. Unapopitia na kusoma vitabu za injili na matendo ya mitume kuhusu batizo, inaonyesha kenye ilikua inahitajika ni mtu kuwa mwanafunzi wa Yesu ama wa Yohana mbatizaji (kwa vitabu nne za injili) ama kuwa mkristo wa kimungu( kwa kitabu cha matendo ya mitume), mkristo wa kimungu ni Yule ambaye alikua anahubiri na kueneza habari njema ya wokovu kwa imani ndani ya Yesu Kristo na damu yake iliyomwagika msalabani. Kwa kuamini hizi habari njema za wokovu, watu walikua wanajitolea ama kutaka kubatizwa.

Baadhi ya mifano kuhusu wakristo wa kimungu katika kitabu cha Matendo wa mitume ni: Petero pamoja na mitume walibatiza umati katika kitabu cha Matendo ya mitume 2 wakijibu ujumbe kuhusu Kristo. Baadae,Filipo,ambaye apo awali alikua amechaguliwa kugawa chakula kwa wajane waliokuwa kanisani uko Yerusalemu, alihubiri injili Samaria na akabatiza waumini uko (Matendo ya mitume 6,8). Badae, Paulo alibatiza wale wote ambao walimwamini Kristo akiwa kwenye kazi yake ya utumwa, lakini pia aliruhusu wengine kufanya ubatizo badala yake (Matendo ya mitume 16:33; Wakoritho ya kwanza 1:10-17)

Kifungu muhimu ambacho kinajaribu kujibu swali hili kinapatikana kwa fungu la 'tume kuu' (Mathayo 28:18-20). Kifungu hiki kimerekodi ile sheria Yesu alipeana ya kutengeneza wanafunzi wa mataifa yote na wabatizwe kama njia moja ya kupata wokovu. Ikiwa tume hii itapeanwa kwa kila mkristo (jinsi hufanyika) hivyo ina maana kuwa uwezo wa kubatiza umepeanwa kwa kila mkristo.

Nyaraka mingi hazijaelezea ni nani anafaa kubatiza badala yake zimeelezea maana fiche ya kupata batizo. Katika kitabu cha Matendo ya mitume na nyaraka, kuelewa vizuri jinsi mtu anapata wokovu( Matendo ya mitume 19:1-5) na zile ishara ambazo zinaonyeshwa na batizo (Warumi) zinaonekana kuwa muhimu kuliko mwenye anafanya batizo.

Kulingana na Mathayo 28:18-20, pamoja na maandiko mengine ambayo hayajaelezea wazi kuhusu swala hili, inaonekana kwamba mkristo yeyote amepewa uwezo wa kubatiza kutoka kwa Mungu pamoja na uwezo wa kueneneza na kufunza yale yote ambayo Kristo alinena.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nani anaruhusiwa kubatiza au kufanya ubatizo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries