settings icon
share icon
Swali

Je! Tunapaswa kubatiza kwa jina la Yesu (Matendo 2:38), au katika jina la Baba, Mwana, an Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19)?

Jibu


Katika siku ya Pentekote, Petro aliambia umati, "Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu" (Matendo 2:38). Amri Yake kuhusu ubatizo ilikuwa ifanyike "kwajina la Yesu Kristo." Mapema Yesu alikuwa amewaambia wanafunzi wake wabatize "kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" (Mathayo 28:19). Tofauti katika maneno imewafanya wengi kuuliza, "Je! Ni mtindo upi ulio bora? Je! tunapaswa kubatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; au tunapaswa kubatiza kwa jina la Yesu pekee?"

Ufafanuzi mmoja unaonyesha ukweli kwamba Baba, Mwana, na Roho ni "utatu katika mwili mmoja." Kubatizwa kwa jina la Mtu mmoja wa Uungu ni sawa na kubatizwa kwa jina la wote watatu. Lakini kuna maelezo mengine zaidi, ambayo inazingatia watazamaji kwa kila amri.

Wakati Yesu alipeana utume mkuu, Alikuwa anawatuma wafuasi wake katika mataifa ili kuwafanya wanafunzi "matiafa yote" (Mathayo 28:19). Katika mataifa ya kikafiri, wangekutana na wale ambao hakuwa wanajua chochote kuhusu Mungu mmoja ambaye ni wa kweli, watu waabudu sanamu ambao walikuwa "hamna tumaini wala Mungu duniani" (Waefeso 2:12). Katika kuihubiri Injili kwa watu kama hao, mtume analazimika kujumlisha mafundisho ya jinsi Mungu anavyoonekana, hii ikiwa ni Pamoja na asili yake ya utatu. (Kumbuka Habari ya kimsingi ambayo Paulo anaanza nayo katika kuwahutubia Waathene katika Matendo 17.) Wale waliopokea injili na kubatizwa watakombolewa kwa mfumo wa dini uliyo tafauti na kukumbatia uelewevu mpya wa kile Mungu alicho.

Kwa ulinganisho, Petro alikuwa akiongea Siku ya Pentekote kwa watu waaminifu wa Kiyahudi ambao tayari walikuwa na uelewo wa Mungu Baba na Roho wa Mungu. Sehemu ya mlingano ambao walikuwa wanakosa ni Yesu, Mwana wa Mungu — na bila Yesu, hawangeweza kuokolewa (Matendo 4:12). Katika kuwasilisha injili kwa Wayahudi, Petro anawaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu; Hiyo ni kusema kwamba, waonyeshe imani kwa yule waliyemsulubisha. Walikuwa wamekiri Baba na Roho, lakini walihitaji kumkiri Mwana. Wale ambao waliipokea injili siku hiyo walijitolea kwa utawala wa Yesu. Hawakumkataa tena bali walimkubali kama Masihi wao na Tumaini tu la wokovu.

We should probably consider the standard formula for Christian baptism to be in the name of the Father, Son, and Holy Spirit. Peter's emphasis on the name of Jesus is understandable, given that he was speaking to the very same Jews who had before rejected and denied Jesus as their Messiah.

Ujumbe wa injili bado unabadilisha maisha hii leo. Wale ambao wanaweka imani yao kwa Yesu Kristo bado wanapokea karama ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Baba. Na ubatizo wa maji bado ni njia iliyowekwa naye Mungu ya kufanya hadharani kukiri imani, kujitambulisha sisi wenyewe na kifo cha Kristo, kuzikwa kwake, na ufufuo wake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunapaswa kubatiza kwa jina la Yesu (Matendo 2:38), au katika jina la Baba, Mwana, an Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries