settings icon
share icon
Swali

Je! Kuba ya Mwamba ni nini?

Jibu


Kuba ya Mwamba ni madhabahu ya Kiislam yaliyojengwa kwenye Mlima wa Hekalu huko Yerusalemu katika AD 691. Kuba ya Mwamba ni sehemu ya eneo kubwa takatifu la Kiislamu ambalo linachukua sehemu kubwa ya kile kinachojulikana pia kama Mlima Moria katika moyo wa Yerusalemu. Kuba ya Mwamba hupata jina lake kutokana na ukweli kwamba imejengwa juu ya sehemu ya juu sana (kuba) ya Mlima Moria ambapo ni mahali Wayahudi na Wakristo wanaamini kwamba Ibrahimu alikuwa tayari kutoa mwanawe Isaka kama dhabihu kwa Mungu (Mwanzo 22:1-14).

Pia inachukuliwa kuwa ni mahali pa uga la Arauna, Myebusi, ambapo Daudi alijenga madhabahu kwa Bwana (2 Samweli 24:18). Pia kwenye eneo au karibu na eneo ambalo Hekalu ya Herode ilisimama kabla kuharibiwa mnamo AD 70 na jeshi la Kirumi. Wengine hata wanaamini kuwa mwamba huenda ukawa mahali Patakatifu pa Watakatifu ambayo ilikuwa ni sehemu ya Hekalu la Kiyahudi ambapo Mkuhani Mkuu wa Kiyahudi angeingia mara moja kwa mwaka ili kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za Israeli.

Kuba ya Mwamba ni sehemu ya eneo kubwa la Kiislamu linalojulikana kama Madhabahu Sharifu au Al-Haram al-Sharif. Eneo hili linajumuisha zaidi ya ekari 35 na ina Msikiti wa Al-Aqsa na Kuba ya Mwamba. Baada ya Waislamu kuchukua udhibiti wa Yerusalemu mnamo AD 637, viongozi wa Kiislamu waliagiza ujenzi wa Kuba ya Mwamba mnamo AD 685. Ilichukua karibu miaka saba kukamilisha na leo ni mojawapo ya majengo ya kiislamu ya kale kabisa duniani.

Jukwaa au eneo la Mlima wa Hekalu ambamo manyumba ya Kuba ya Mwamba na Msikiti Al-Aqsa yalijengwa katika karne ya kwanza AD chini ya utawala wa Herode Mkuu kama sehemu yake ya kujenga upya Hekalu la pili la Wayahudi. Yesu aliabudiwa katika Hekalu la Herode, na pale ndipo alitabiri uharibifu wake (Mathayo 24:1-2). Unabii wa Yesu ulitimizwa wakati Hekalu liliharibiwa na jeshi la Kirumi mnamo AD 70.

Eneo la Mlima wa Hekalu ambapo Kuba ya Mwamba imewekwa ni muhimu sio tu kwa Waislamu ambao wanaudhibiti sasa, lakini pia kwa Wayahudi na Wakristo. Kama mahali ambapo Hekalu ya Wayahudi ilisimama wakati mmoja, Mlima wa Hekalu unachukuliwa kuwa mahali patakatifu zaidi katika Uyahudi na ni mahali ambapo Wayahudi na Wakristo wengine wanaamini kwamba hekalu ya tatu na ya mwisho itajengwa. Eneo hili pia ni eneo la tatu takatifu zaidi katika Uislamu. Kwa sababu ya umuhimu wake kwa Wayahudi na Waislamu, eneo la Mlima wa Hekalu ni eneo la kidini linalopiganiwa sana ambayo Mamlaka ya Palestina na Israeli wanadai utawala.

Kuba ya Mwamba ni muundo wa kuvutia, unaonekana kwa urahisi katika picha nyingi za Yerusalemu. Sio tu uko juu ya Mlima Moria, lakini pia ulijengwa juu ya jukwaa lililoinuliwa na kuinua hadi futi 16 zingine juu ya sehemu nyingine ya Mlima wa Hekalu. Ndani ya katikati ya Kuba ni sehemu ya juu zaidi ya Mlima Moria. Mwamba huu tupu una vipimo vya futi 60 na futi 40 na inainuka karibu na futi 6 kutoka kwa sakafu ya madhabahu. Huku watu wengi kimakosa wanarejelea Kuba ya Mwamba kama msikiti, kwa kweli ilijengwa kama madhabahu kwa haji, ingawa imewekwa karibu na Msikiti muhimu wa Kiislamu.

Wengine wanaamini kwamba Kuba ya Mwamba ilijengwa kwa sababu, kwa mujibu wa hekaya ya Waislamu, Mtume Muhammad alipelekwa Mlima Moria na Malaika Gabrieli na kutoka hapo akapaa mbinguni na akakutana na manabii wote waliomtangulia, pamoja na kumwona Mungu ameketi juu ya kiti Chake cha enzi akizungukwa na malaika. Hata hivyo, hadithi hii haionekani katika maandiko yoyote ya Kiislamu mpaka miongo kadhaa baada ya madhabahu kujengwa, ambayo liliwaongoza wengine kuamini sababu ya msingi kwamba Kuba ilijengwa kusherehekea ushindi wa Kiislamu juu ya Wakristo huko Yerusalemu na sio kuheshimu madai ya upaaji wa Muhammad.

Wakati Waisraeli walichukua udhibiti juu ya sehemu hiyo ya Yerusalemu baada ya Vita vya Siku sita mwaka 1967, viongozi wa Israeli waliruhusu uaminifu wa kidini ya Kiislamu kuwa na mamlaka juu ya Mlima wa Hekalu na Kuba ya Mwamba kama njia ya kusaidia kuweka amani. Tangu wakati huo wasio Waislamu wameruhusiwa ufikiaji mdogo wa eneo lakini hawaruhusiwi kuomba kwenye Mlima wa Hekalu.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuba ya Mwamba ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries