settings icon
share icon
Swali

Mwanakondoo wa Pasaka ni nani? Ni namna gani Yesu ni Mwanakondoo wa Pasaka?

Jibu


Kondoo wa pasaka alikuwa mnyama ambaye Mungu aliamrisha Waisraeli kutumia kama dhabihu kule Misri usuku ule Mungu aliwaua vitinda mimba/wazaliwa wa kwanza wa kila nyumba (Kutoka 12:29). Hili lilikuwa pigo la mwisho Mungu alitoa dhidi ya Farao, na ilimsababisha Farao kuwaachilia Waisraeli kutoka utumwani (Kutoka 11:1). Baada ya usiku huo wa mkasa, Mungu aliwaamuru Waisraeli kuadhimisha Pasaka kama siku kuu (Kutoka 12:14).

Mungu aliamuru kila nyumba ya Mwisraeli kuchagua mwana-kondoo wa kiume aliye wa mwaka mmoja na asiye na duwaa lolote (Kutoka 12:5; tazama pia Walawi 22:20-21). Kila kiongozi wa kila nyumba alikuwa amchinje huyo kondoo majira ya mapambazuko, na akiakisha kuwa hamna mfupa amevunjwa, na kupaka sehemu ya damu katika milingoti ya juu na kando ya mlango ya nyumba. Kikondoo huyo alipaswa kuchomwa na kuliwa (Kutoka 12:7-8). Mungu pia alipeana maagizo maalumu ya jinsi Waisraeli walipaswa kumla kikondoo huyo, "Mtakuwa mmejifunga mikanda viunoni mwenu, mmevaa viatu na fimbo zenu mikononi" Kutoka 12:11). Kwa maneno mengine, walipaswa kuwa tayari kusafiri.

Mungu alisema ya kwamba wakati ataona damu katika milingoti ya mlango, Atapita nyumba hiyo na asiruhusu "mwangamizi" kuingia (Kutoka 12:23). Nyumba yoyote yenye haikuwa na damu ya kijikondoo atapata watoto wao vitindamimba watauwawa usiku huo (Kutoka 12:12-13).

Agano Jipya linweka uhusiano kati ya kielezo hiki ya kijikondoo wa Pasaka na Kondoo timizi wa Pasaka, Yesu Kristo (1 Wakorintho 5:7). Nabii Yohana mbatizaji alimtambua Yesu kama "Mwanakondoo wa Mungu (Yohana 1:29), na mtume Petro anafungamanisha kondoo asiye na ulemavu wowote (Kutoka 12:5) na Kristo ambay anamwita "ambaye alikuwa kama mwanakondoo asiye na dosari wala doa" (1Petro 1:19). Yesu anastahili kuitwa mmoja "asiye na dosari" kwa sababu maisha yake hayakuwa na dhambi (Waebrania 4:15). Katika Ufunuo, mtume Yohana anamwona Yesu kama "Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwamba amechinjwa" (Ufunuo 5:6). Yesu alisulubiwa wakati Pasaka ilikuwa inaadhimishwa (Marko 14:12).

Biblia inasema kuwa waumini kimfano wanatumia damu ya Yesu ya dhabihu mioyoni mwao na hivyo kukwepa kifo cha milele (Waebrania 9:12,14). Kama vile damu ya kijikondoo wa Pasaka iliyopakwa ilimsababisha "muuaji" kupita kila nyumba, vile vile damu ya Krisot iliyotumika inafanya hukumu ya Mungu kumpita mwenye dhambi na kumpa maisha muumini (Warumi 6:23).

Kama vile Pasaka ya kwanza inaashiria kuachiliwa kwa Waebrania kutoka utumwani Mistri, vile vile kifo cha Kristo kinaashiria kufunguliwa kutoka utumwa wa dhambi (Warumi 8:2). Kama vile pasaka ya kwanza ilistahili kuwa ukumbusho kama siku kuu ya kila mwaka, hivyo Wakristo wanastahili kukumbuka kifo cha Bwana kupitia meza ya Bwana hadi atakaporudi (1 Wakorintho 11:26).

Kijikondoo cha Pasaka ya Agano la Kale, ingawa ilikuwa kawaida wakati huo, ilikuwa ni kuvuli cha Kondoo wa Pasaka njema ya mwisho, Yesu Kristo. Ingawa maisha yake yasiyo ya dhambi na kifo cha dhabihu, Yesu akawa ndiye pekee awezaye kuwapa watu njia ya kutoroka kifo na akikisho la tumaini la maisha ya milele (1Petro 1:20-21).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mwanakondoo wa Pasaka ni nani? Ni namna gani Yesu ni Mwanakondoo wa Pasaka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries