settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kuwa kizuizi kwa mtu mwingine?

Jibu


Katikati ya mfululizo wa sheria zinazozungumzia kushiriki na wengine, tunaona "Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi Bwana."(Mambo ya Walawi 19:14). Kwa wazi, kuweka mwamba au matofali mbele ya kipofu ni ukatili, lakini Agano Jipya huchukua mfano huu na kugeuza kuwa mfano wa kiroho.

Baada ya Petro kumkemea Yesu, na kukataa kwamba kusulubiwa kungetokea, Yesu alisema, "Nenda nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu; kwa maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. "(Mathayo 16:23). Petro, chini ya ushawishi wa Shetani, alijaribu kumzuia Yesu kutokana na kile alichokuja anafanya. Alijaribu kumfanya Yesu "arudi nyuma" katika harakati za kusulubiwa. Paulo anaelezea wazo hili: "... bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi." (1 Wakorintho 1:23). Wazo kwamba Masihi angesulubishwa ilikuwa ni kikwazo kwa Wayahudi-kitu ambacho kilichochochea imani zao kuhusu kile ambacho Masihi angekuwa.

Lakini mara nyingi, "kizuizi" kinamaanisha kitu au mtu anayemfanya mwingine kutoka kwa uhusiano wake na Mungu. Katika Mathayo 18: 5-7, Yesu anasema, "Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.

Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha! "Kama vile ingekuwa bora kukata mkono kuliko kufanya dhambi (Mathayo 18: 8), katika mtazamo wa Ufalme, ingekuwa bora kuzama kuliko kuongoza mtoto kufanya dhambi. Vivyo hivyo, katika Warumi 14:13, Paulo anasema kuwa Mungu peke yake ndiye anahukumu; hatupaswi kuwahukumu wengine lakini tuhakikishe kwamba sio sisi tunawaongoza katika dhambi ambayo hututia wasiwasi sana.

Vikwazo pia hutokea wakati njia ni ndogo zaidi. Maisha komavu ya Kikristo inaruhusu uhuru fulani unaoonekana kinyume na imani tiifu, na yenye nidhamu. Wakorintho walikuwa na wasiwasi kuhusu kula nyama iliyotolewa kwa sanamu. Masuala tata ya kisasa siku hizi ni pamoja na kunywa pombe kwa kiasi au kunengua viungo. "Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu" (1 Wakorintho 8: 9). Uhuru wetu hautoshani na kutembea kwa mtu mwingine na Mungu. Ikiwa kitu ambacho Mungu anaruhusu kinaweza kuongoza mwingine kufanya dhambi, tunahitaji kukiepuka. Tunapewa uhuru mkubwa kama Wakristo, lakini kubwa ni uhuru wa kuzingatia ustawi wa wengine zaidi yetu wenyewe.

Kujiepusha kutoka kuwa kizuizi inamaanisha kutoongoza mwingine katika dhambi. Jinsi tunavyotimiza hili inategemea hali na mioyo ya wale walio karibu nasi. Usalama tunao katika upendo wa Mungu na utunzaji wake, wote sasa na milele, unatuwezesha kuonyesha jinsi tunavyo hisi kwa wale walio dhaifu-wale wanaohitaji faraja maalum kuelewa Mungu ni nani. Katika hali fulani, hiyo inamaanisha kuishi katika uhuru huo kuonyeshe kwamba Mungu ni Mungu wa neema. Kwa wengine, inamaanisha kujitenga wenyewe kwa kujenga waumini dhaifu na si kuwafukuza katika uhuru ambao hawajawa tayari. Lakini, daima, inamaanisha kuwa si kuhimiza mwingine kutenda kama njia Biblia inatambua kuwa dhambi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kuwa kizuizi kwa mtu mwingine?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries