settings icon
share icon
Swali

Je, kizazi kilichoona Israeli ikiundwa tena kama taifa bado wakuwa hai kwa ajili ya kuja kwa pili?

Jibu


Dhana hii kwa kawaida inatolewa Mathayo 24:34, "Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia." Aya zilizopita, Mathayo 24: 1-33, zinaelezea matukio ya wakati wa mwisho kwa mjibu wa Israeli. Matokeo yake, baadhi ya wakalimani walidhani kuwa nyakati za mwisho zitaanza wakati Waisraeli "walipatanishwa" kama taifa (kilichotokea mwaka wa 1948). Hata hivyo, kama muda zaidi na zaidi umepita tangu mwaka wa 1948, muda uliofunikwa na "kizazi" umepaswa kupanuka na kupanuka. Imekuwa sasa zaidi ya miaka 60-ambayo ni zaidi ya ufafanuzi wa kawaida wa kizazi.

Tatizo kubwa na mafundisho haya ni kwamba Mathayo 24 haitajaja kuundwa upya kwa Israeli au kutupa hatua yoyote ya kuanzia kwa kuhesabu miaka ya "kizazi." Chenye mkudhatha unaonekana kusema ni kwamba, mara matukio ya mwisho yanaanza kutokea, yatatokea haraka. "Kizazi hiki" ni kizazi kilicho hai wakati wa "mwanzo wa maumivu" (mstari wa 8); mara moja shida itakapoanza, mambo yatatokea kwa mfululizo wa haraka.

Maneno ya unabii ya Yesu katika Mathayo 24 yanaweza pia kuwa "kutimizo mara mbili." Baadhi ya matukio yalitokea AD 70 wakati Warumi waliharibu Yerusalemu. Matukio mengine (katika mstari wa 29-31, kwa mfano) bado hayajawahi. Baadhi ya maneno ya Yesu yalitimizwa muda mfupi baada ya kuwaambia (ndani ya kizazi chake); wengine hayatatimizwa mpaka kizazi cha mwisho cha nyakati kimekuwepo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kizazi kilichoona Israeli ikiundwa tena kama taifa bado wakuwa hai kwa ajili ya kuja kwa pili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries