settings icon
share icon
Swali

Hiki kiti cheupe cha hukumu ndio gani?

Jibu


Kiti cheupe cha hukumu kimeelezwa katika ufunuo Wa Yohana 20:11-15 na ndio hukumu ya mwisho kabla ya wenye dhambi kutupwa katika ziwa la moto. Tunajua kutoka ufunuo 20:7-15 ya kwamba hukumu itafanyika baada ya kipindi cha miaka elfu moja na baada ya Shetani, mnyama na nabii wa uongo wametupwa katika ziwa la moto (Ufunuo Wa Yohana 20:7-10). Vitabu vile ambavyo vimefunguliwa (Ufunuo 20:12) viko na rekodi ya kila mmoja na matendo yake, hata kama yalikuwa mazuri au mabaya, kwa sababu Mungu anajua kila kitu ambacho kimesemwa, kutendwa au hata mawazo, atatuza au kuadhibu kila mtu kulingana na matendo yake (Zaburi 28:4; 62:12; Warumi 2:6; Ufunuo 2:23; 18:6; 22:12).

Pia kwa wakati mwingine, kitabu kingine kimefunguliwa, nacho kinaitwa “kitabu cha uzima” (Ufunuo 20:12). Ni ndani ya kitabu hiki kinachoamua ikiwa ataurithi uzima wa milele na Mungu au atapokea hukumu ya milele katika ziwa la moto. Ingawa Wakristo watawajibika kwa matendo yao, wamesamehewa katika Kristo na “majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu” (Ufunuo 17:8). Pia tunajua kutoka maandiko kuwa ni katika hii hukumu wafu “watahukumiwa kulingana na matendo yao” Ufunuo 20:12) na kwamba “yeyote ambaye jina lake halitapatikana katika “kitabu cha uzima” atatupwa “katika lile ziwa la moto” (Ufunuo 20:15).

Dhana kwamba kutakuwa na hukumu ya mwisho kwa wanadamu wote, Wakristo and wasio wakristo imethibitwa wazi katika fahamu nyingi za maandiko. Kila mtu siku moja atasimama mbele ya Kristo na kuhukumiwa kwa matendo yake. Na vile ilivyo wazi kiti kikuu cheupe hukumu hii ndio ya mwisho, Wakristo wanatofautiana na vile kimehusiana na hukumu nyingine ambayo imetajwa katika Bibilia hasa ni nani atakaye hukumiwa katika kiti cheupe cha hukumu.

Baadhi ya Wakristo wengine wanaamini kuwa maandiko yanafunua hukumu tatu peke ambazo zitakuja. Ya kwanza ni hukumu ya mbuzi na kondoo au hukuma ya mataifa (Mathayo 25:31-36). Hii itafanyika baada ya kipindi cha matezo kabla ya ufalme wa miaka elfu moja; lengo lake ni kutambua ni nani atakayeingia katika ufalme wa miaka elfu moja. Hukumu ya pili ya kazi ya Mkristo, kila mara inarejelewa kwetu kama “kiti cha hukumu cha Kristo” (2 Wakorintho 5:10). Katika hii Wakristo watapokea kiwango cha tuzo la matendo yao. Tatu ni kile kiti kikuu cheupe cha hukumu kile kiti cheupe cha hukumu katika mwisho wa ufalme wa miaka elfu moja (Ufunuo 20:11-15). Hii ni hukumu ya wale wasio Wakristo ambayo watahukumiwa kulingana na kazi yao na kuhukumiwa ile hukumu ya ziwa la moto.

Wakristo wengine wanaamini kuwa hizi hukumu tatu zinazungumzia hukumu moja ile ya mwisho, sio hukumu tatu tofauti. Kwa njia nyingine, kile kiti kikuu cheupe cha hukumu katika Ufunuo 20:11-15 utakuwa wakati Wakristo na wasio Wakristo watahukumiwa pamoja. Wale majina yao yatapatikana katika kitabu cha uzima watahukumiwa kwa matendo yao ili tuzo ikadiriwe watakayoipata au watakayoipoteza. Wale ambao majina yao hayataonekana katika kitabu cha uzima watahukumiwa kulingana na matendo yao ili tuzo kamili la hukumu likadiriwe watakayoipokea katika ziwa la moto. Wale wanaoshikilia mtazamo huu wanaamini kuwa Mathayo 25:31-46 ni elezo lingine la yale yatakayotokea katika kiti kikuu cheupe. Hoja kwa pointi kwamba matunda ya hukumu yatakuwa yale yale kwa ile inayoonekana baada ya kiti cheupe cha hukumu katika Ufunuo 20:11-15. Kondoo (Wakristo) wanaingia katika uzima wa milele, bali mbuzi (wasio Wakristo) watatupwa katika “hukumu” ya milele (Mathayo 25:46).

Mtazamo wowote mtu anaweza shikilia wa kile kiti cheupe cha hukumu, ni muimu kutosahau ile hukumu ijayo. Kwanza Yesu Kristo atakuwa hakimu, wote wasiomwamini watahukumiwa naye, na wataadhibiwa kulingana na matendo yao wametenda. Bibilia ii wazi kuwa wasio Wakristo wanajiwekea ghadhabu wao wenyewe (Warumi 2:6) na kwamba Mungu “atakayemlipa kila mtu kwa dadiri ya matendo yake” (Warumi 2:6). Wakristo pia watahukumiwa na Kristo, lakini tangu utakatifu wa Kristo umapachikwa kwetu na majina yutu yameandikwa katika kitabu cha uzima, tutatuzwa, bali hatutahukumiwa kulingana na matendo yetu. Warumi 14:10-12 yasema kwamba zote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo na kila mtu tatoa hesabu ya matendo yake kwa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Hiki kiti cheupe cha hukumu ndio gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries