settings icon
share icon
Swali

Kiti cha hukumu cha Kristo ni kipi?

Jibu


Warumi 14:10-12 yasema, “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.” Wakorintho wa Pili 5:10 yatuambia, “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” Kwa muktadha huu, ni wazi kuwa maandiko yote yanahusu Wakristo, sio wasio Wakristo. Kiti cha hukumu cha Kristo, kwa hivyo kinahuzisha Wakristo kutoa hesabu ya maisha yao kwa Kristo. Kiti cha hukumu cha Kristo hakitambui wokovu; hiyo ilithibitishwa na kusulubiwa kwa Yesu kwa niaba yetu (1 Yohana 2:2) na imani yetu kwake (Yohana 3:16). Dhambi zetu zote zimesamehewa na hatutahukumiwa kwa sababu yao (Warumi 8:1). Hatustahili kuangalia katika kiti cha hukumu cha Kristo kuwa ni Mungu anazihukumu dhambi zetu, bali kuwa ni Mungu anatuzawadi kwa maisha yetu. Naam, vile Bibilia inasema, tutatoa hesabu sisi wenyewe. Sehemu ya hii ni kwa kweli ni kuzijibu baadhi ya dhambi zetu ambazo tulizitenda. Ingawa, hiyo haitakuwa jambo la kimsingi kuangazia kiti cha hukumu cha Kristo.

Katika kiti cha hukumu cha kristo, Wakristo watalipwa kulingana na vile walimtumikia Kristo kwa uaminifu (1 Wakorintho 9:4-27; 2 Timotheo 2:5). Baadhi ya vitu vingine tunaweza hukumiwa ni vile tulivyo tii jukumu kuu la kuihubiri injili (Mathayo 28:18-20), vile tulikuwa washindi kwa dhambi (Warumi 6:1-6), na vile tulizuia ndimi zetu (Yakobo 3:1-9). Bibilia inazungumzia Wakristo kupokea taji kwa mambo tofauti kulingana na vile walimtumikia Kristo kwa uaminifu (1 Wakorintho 9:4-27; 2 Timotheo 2:5). Taji tofauti zimeelezewa katika 2 Timotheo 2:5, 2 Timotheo 4:8, Yakobo 1:12, 1 Petero 5:4 na Ufunuo 2:10. Yakobo 1:12 ni muhtasari mzuri wa vile tunastahili kufikiria juu ya kiti cha hukumu cha Kristo: “Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kiti cha hukumu cha Kristo ni kipi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries