settings icon
share icon
Swali

Je! Katibu cha Mafundisho cha Wayahudi ni nini?

Jibu


Neno "Talimudi/Kitabu cha Mafundisho cha Wayahudi" ni neno la Kiyahudi linalomaanisha "Mafunzo, maagizo." Kitabu cha Mafundisho cha Wayahudi ni andiko kiungo katika Uyahudi halisi na kinajumuisha jadilio la kimsingi na maelezo juu ya historia ya Kiyahudi, sheri (haswa matumizi yake katika maisha), desturi na tamaduni. Kitabu cha Mafundisho cha Wayahudi kina kile kijulikanajo kama Gemara na Mishnah.

Zaidi ya maandiko yalivuviwa ya Kiebrania, ambayo Wakristo wanayaita Agano la Kale, Uyahudi una "Torah ya mdomo" ambayo ni utamaduni wa kuelezea kile maandiko yanamaanisha na jinsi ya kuyatafsiri na kutumia sheria. Wayahudi halisi wanaamini kuwa Mungu alifundisha Torati hii ya Mdomo kwa Musa, na wengine wanaamini hivyo hadi leo hii. Utamaduni huu ulidumishwa tu kwa njia ya mdomo hadi karibu karne ya 2 BK, wakati sheria ya mdomo ilipokusanywa na kuandikwa katika hati iliyoitwa Mishnah. Katika karne zinginie chache zilizofuata, ufafanuzi wa ziada uliofafanua Mishnah uliandikwa huko Yerusalemu na Babeli. Ufafanuzi huu wa ziada hujulikana kama Gemara. Gemara na Mishnah pamoja hujulikana kama Talimudi. Hii ilikamilishwa katika karne ya 5 BK.

Kwa kweli kuna Talimudu mbili: Talimudi ya Yerusalemu na Talimudi ya Babeli. Talimudi ya Babeli ni ya upana zaidi, na ndio watu wengi wanamaanisha ikiwa watasema "Talimudi" bila kutaja ni ipi hasa. Talimudi si rahisi kuisoma. Mara nyingi kuna upungufu katika hoja zake ambapo hudhaniwa kuwa tayari unakijua chenye wanazungumzia, na dhana mara nyingi huonyeshwa kwa aina ya dhana. Mistari ya kibiblia inayounga mkono mafundisho mara nyingi hurejelewa na maneno mawili au matatu tu. Talimudi inahifadhi maoni anuwai juu ya kila suala na haionyeshi wazi wazi ni maoni gani yanayokubalika.

Ukristo hauichukulii Talimudi kuwa imevuviwa kwa maana ile ile ya vitabu 66 vya kanuni za kibiblia kuwa na "pumzi ya" (2 Timotheo 3:16). Ingawa baadhi ya mafundisho mengine kutoka kwa Talimudi inaweza "kuambatana" na mafundisho ya kibiblia, hiyo pia inaweza kusemwa kwa maandishi mengi tofauti kutoka kwa dini zingine nyingi tofauti. Kwa Mkristo, kuichunguza Talimudi inaweza kuwa njia nzuri ya kujifunza zaidi juu ya mila ya Kiyahudi, historia, na ufafanuzi, lakini Talimudi haipaswi kuzingatiwa kuwa Neno la Mungu lenye mamlaka.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Katibu cha Mafundisho cha Wayahudi ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries