settings icon
share icon

Kitabu cha Yoshua

Mwandishi: Kitabu cha Yoshua hakifafanui jina la mwandishi wake. Kuna uwezekano zaidi kuwa Yoshua mwana wa Nuni, mrithi wa Musa kama kiongozi wa Israeli, aliandika mengi ya kitabu hiki. Sehemu ya mwisho ya kitabu kiliandikwa na mtu mwingine angalau mmoja baada ya kifo cha Yoshua.Pia kuna uwezekano kwamba sehemu kadhaa zilirekebishwa / kusanywa kufuatia kifo cha Yoshua.

Tarehe ya Kuandikwa: Kuna uwezekano Kitabu cha Yoshua kiliandikwa kati ya 1400 na 1370 BC

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Yoshua kinatoa maelezo ya jumla ya kampeni za kijeshi kushinda eneo la nchi ambayo Mungu aliwahidi. Kufuatia kutoka Misri na baadae miaka arobaini ya kuzunguka jangwani, taifa jipya-lililoundwa sasa lipo katika nafasi ya kuingia katika Nchi ya Ahadi, kuwashinda wenyeji, na kuchukua utawala. Maelezo ya jumla tunayo hapa yanatoa maelezo kwa kifupi na teule ya vita vingi na namna ambavyo nchi si tu ilitawaliwa, bali jinsi ilivyokuwa imegawanywa katika maeneo ya kikabila.

Mistari muhimu: Yoshua 1: 6-9, "Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa. Uwe hodari tu na ushujaaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kiume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapofanikisha njia yako, kasha ndipo utakapositawi sana. Je! Si mimi niliyekuamru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako . "

Yoshua 24: 14-15, "Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na ukweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA. Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA. "

Muhtasari Kwa Kifupi : Kitabu cha Yoshua kinaendelesha historia ya Wana Wa Israeli baada ya kutoka Misri. Kitabu kinarekodi takriban miaka 20 ya uongozi wa Yoshua ya watu baada ya Musa kumteua mwishoni mwa Kumbukumbu La Torati. Migawanyiko ishirini na nne ya Kitabu cha Yoshua kinaweza kuwekwa kimuhtasari kama ifuatavyo.

Sura 1-12: kuingia na kutawala Nchi ya Ahadi.
Sura 13-22: Maelekezo ya kugawanya sehemu za nchi ya ahadi.
Sura 23-24: Hotuba ya Yoshua ya kuagana.

Ishara: Hadithi ya Rahabu aliyekuwa malaya na imani yake kubwa katika Mungu wa Waisraeli ilimpatia nafasi na wale walioheshimiwa kwa imani yao katika Waebrania 11:31. Kwake ni hadithi ya neema ya Mungu kwa wenye dhambi na wokovu kwa imani peke yake. Muhimu zaidi, kwa neema ya Mungu yeye alikuwa katika mstari wa Kimasihi (Mathayo 1:15).

Moja ya sherehe ya matambiko ya Yoshua 5 ilipata kutimizwa vikamilifu katika Agano Jipya. Mistari ya 1-9 inaeleza amri ya Mungu kwamba wale ambao waliozaliwa katika jangwa wangetahiriwa watakapofika katika Nchi ya Ahadi. Kwa kufanya hivyo, Mungu "alibingirisha mbali aibu ya Misri" kutoka kwao, ina maana kuwa yeye aliwasafisha wao kutoka dhambi za maisha yao ya zamani. Wakolosai 2: 10-12 inaeleza waumini wamepashwa tohara katika mioyo yao na Kristo mwenyewe, ambaye kupitia kwake tumetoa maisha ya awali ya dhambi bila Kristo.

Mungu alianzisha miji ya kukimbilia ili wale walioua mtu kiajali wanaweza kuishi huko bila hofu ya kuadhibiwa. Kristo ni kimbilio letu ambaye sisi "tumekimbilia kuchukua umiliki wa matumaini yaliyotolewa kwetu" (Waebrania 6:18).

Kitabu cha Yoshua kina dhamira kinyume ya kiteolojia ya mapumziko. Wana Wa Israeli, baada ya kuzunguka katika jangwani kwa miaka 40, hatimaye waliingia kwa pumziko Mungu alikuwa amewandalia wao katika nchi ya Kanaani. Mwandishi wa Waebrania anatumia tukio hili kama onyo kwetu kutoruhusu kutoamini kutuzuia kuingia katika pumziko la Mungu katika Kristo (Waebrania 3: 7-12).

Vitendo tekelezi: Mojawapo ya mistari muhimu ya Kitabu cha Yoshua ni 1: 8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo”. Agano la Kale limejaa hadithi za namna watu “walisahau” Mungu na Neno lake na kuteseka katika hali ya kutisha. Kwa Mkristo, Neno la Mungu ni uhaidamu wetu. Kama tutalipuusa, maisha yetu yatateseka vilivyo. Lakini kama tutachukua moyoni kanuni ya mstari wa 1: 8, tutakuwa wakamilivu na wenye uwezo wa kuwa wa manufaa katika ufalme wa Mungu (2 Timotheo 3: 16-17), na tutapata kwamba ahadi za Mungu katika Yoshua 1: 8- 9 zitakuwa zetu pia.

Yoshua ni mfano mkuu wa faida ya mshauri wa dhamani. Kwa miaka alikaa karibu na Musa. Yeye alimwangalia Musa akimfuata Mungu kwa namna isiokuwa na dosari. Alijifunza kuomba katika njia binafsi kutoka kwa Musa. Yeye alijifunza jinsi ya kutii kupitia mfano wa Musa. Yoshua bayana pia alijifunza kutokana na mfano hasi uliomgharimu Musa furaha ya kweli ya kuingia Nchi ya Ahadi. Kama wewe ni hai, wewe ni mshauri. Mtu, mahali fulani, anakuangalia wewe. Baadhi ya vijana au mtu ambaye wewe unamshawishi anakuona jinsi unavyoishi na jinsi unavyoonyesha hisia. Mtu anajifunza kutoka kwako. Mtu atafuata mfano wako. Mfano bora umeshinda maneno ambayo yatatamkwa na mshauri. Maisha yake yote yamewekwa wazi.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Yoshua
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries