settings icon
share icon

Kitabu cha Yoeli

Mwandishi: Kitabu cha Yoeli kinanakili kwamba mwandishi wake alikuwa ni Nabii Yoeli (Yoeli 1: 1).

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Yoeli huenda kiliandikwa kati ya 835 na 800 kk

Kusudi la Kuandika: Yuda, msingi wa kitabu, unaharibiwa kwa idadi kubwa ya nzige. Uvamizi huu wa nzige unaharibu kila kitu-mashamba ya ngano, na mizabibu, mabustani na miti. Yoeli kwa mfano anaeleza kuhusu nzige kuwa kama jeshi la binadamu linalotembea na anaoni haya yote kama hukumu takatifu ya Mungu inayokuja dhidi ya taifa kwa ajili ya dhambi yake. Kitabu kinatawaliwa na matukio makubwa mawili. Moja ni uvamizi wa nzige na nyingine ni kumwagwa kwa Roho. Kutimizwa kwa haya awali kulinukuliwa na Petro katika Matendo 2 kama kulifanyika wakati wa Pentekoste.

Mistari muhimu: Yoeli 1: 4, "Yaliyasazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu."

Yoeli 2:25, "Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige ..."

Yoeli 2:28, "Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono."

Muhtasari kwa kifupi: Pigo la kutisha la nzige linafutiwa na njaa kali katika nchi yote. Yoeli anatumia matukio haya kama kichocheo kutuma maneno ya onyo kwa Yuda. Ila tu watu watubu kabisa kwa haraka, majeshi ya adui wameza nchi kana kwamba ni vitu vya asili. Yoeli anawasihi watu wote na makuhani wa nchi kufunga na kujinyenyekeza wanapotafuta msamaha wa Mungu. Ikiwa wataitikia, kutakuwa na kubarikiwa upya kifedha na kiroho kwa taifa. Lakini siku ya Bwana inakuja. Wakati huu nzige waliohofiwa sana watakuwa kama jambo dogo kwa kulinganisha, kama mataifa yote yanapokea hukumu yake.

Mada kuu ya kitabu cha Yoeli ni Siku ya Bwana, siku ya ghadhabu ya Mungu na hukumu. Hii ndiyo Siku ambayo Mungu anaonyesha sifa zake za ghadhabu, nguvu na utakatifu, na ni siku ya kutisha kwa maadui wake. Katika sura ya kwanza, siku ya Bwana inaafikiwa kihistoria na pigo la nzige juu ya nchi. Sura ya 2: 1-17 ni sura ya mpito ambayo Yoeli anatumia mfano wa pigo la nzige na ukame kutoa mwito mpya wa toba. Sura ya 2: 18-3: 21 zinaeleza Siku ya Bwana katika matamshi ya hukumu na kujibu wito wa kutubu na unabii wa Ukombozi wa kimwili (2: 21-27), marejesho ya kiroho (2: 28-32), na urejesho wa kitaifa ( 3: 1-21).

Ishara: Kila wakati Agano la Kale linazungumzia hukumu ya dhambi, hata kama ni dhambi za mtu binafsi au dhambi za kitaifa, ujio wa Yesu Kristo unaashiriwa.Manabii wa Agano la Kale waliendelea kuonya Israeli watubu, bali hata walipotubu, toba yao iliazimiwa kwa kazi na utunzaji wa sheria. Sadaka zao za hekalu zilikuwa tu kivuli cha sadaka ya mwisho, inayotolewa mara moja kwa wakati wote, ambayo itakuja katika msalaba (Waebrania 10:10). Yoeli anatuambia kwamba hukumu ya mwisho ya Mungu, ambayo iko katika Siku ya Bwana, itakuwa "kubwa na ya kutisha. Nani anaweza kuivumilia? "(Yoeli 2:11). Jibu ni kwamba sisi, juu yetu wenyewe, hatuwezi kamwe kuvumilia wakati kama huo. Lakini kama tumeweka imani yetu katika Kristo kwa ajili ya upatanisho wa dhambi zetu, hatuna lolote la kuogopa kutokana na Siku ya Hukumu.

Vitendo Tekelezi: Bila kutubu, hukumu itakuwa kali, kamilifu na yakini. Matumaini yetu yasiwe katika mali zetu bali katika Bwana Mungu wetu. Mungu nyakati zingine anaweza kutumia asili, huzuni au matukio mengine ya kawaida kwa kutuvuta karibu naye. Lakini katika rehema yake na neema, Yeye ametoa mpango thabiti kwa ajili ya wokovu wetu - Yesu Kristo, aliyesulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu na kubadilishana dhambi zetu na haki yake kamilifu (2 Wakorintho 5:21). Hakuna muda wa kupoteza. Hukumu ya Mungu itakuja haraka, kama mwizi usiku (1 Wathesalonike 5: 2), na lazima tuwe tayari. Leo ni siku ya wokovu (2 Wakorintho 6: 2). "Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa "(Isaya 55: 6-7). Ni tu kwa kujitwalia wokovu wa Mungu tunaweza kuepuka ghadhabu yake katika Siku ya Bwana.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Yoeli
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries