settings icon
share icon

Kitabu cha Yeremia

Mwandishi: Yeremia sura ya 1, mstari wa 1 unatambua nabii Yeremia kama mwandishi wa Kitabu cha Yeremia.

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Yeremia kiliandikwa kati ya 630 na 580 kk

Kusudi la Kuandika: Kitabu cha Yeremia kinanakili unabii wa mwisho kwa Yuda, ukionya kuhusu uharibifu utakaokuja ikiwa taifa halitatubu. Yeremia anatoa wito kwa taifa lirudi kwa Mungu. Wakati huo huo, Yeremia anatambua uharibifu usioepukuka wa Yuda kutokana na kuabudu sanamu na uasherati bila kutubu.

Mistari muhimu: Yeremia 1: 5 "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; Nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. "

Yeremia 17: 9, "Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; Nani awezaye kuujua? Yeremia 29: 10-11, Maana Bwana asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa. Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyti, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. '"

Yeremia 52: 12-13, "Basi katika mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na kenda wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, amirĂ­ wa askari walinzi, aliyesimama mbele ya mfalme wa Babeli, aliingia Yerusalemu.Akaiteketeza nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, Kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto. "

Muhtasari kwa kifupi: Kitabu cha Yeremia kimsingi ni ujumbe wa hukumu juu ya Yuda kwa ajili ya kuabudu sanamu kulioenea kote(Yeremia 7: 30-34, 16: 10-13; 22: 9; 32:29; 44: 2-3). Baada ya kifo cha Mfalme Yosia, mfalme wa mwisho wa haki, taifa la Yuda lilikuwa limemwacha kabisa Mungu na amri zake. Yeremia analinganisha Yuda na malaya (Yeremia 2:20; 3: 1-3). Mungu alikuwa ameahidi kwamba atahukumu kuabudu sanamu vibaya zaidi (Mambo ya Walawi 26: 31-33, Kumbukumbu 28: 49-68), na Yeremia alikuwa akiionya Yuda kwamba hukumu ya Mungu ilikuwa imekaribia. Mungu alikuwa ameokoa Yuda kutokana na uharibifu mara kadhaa, lakini huruma yake ilikuwa katika mwisho wake. Yeremia anarekodi mfalme Nebukadreza kuwa ataitawala Yuda na kuifanya iwe chini yake (Yeremia 24: 1). Baada ya uasi zaidi, Mungu akaleta Nebukadreza na majeshi ya Babeli kuharibu na kutia ukiwa/uzuni katika Yuda na Yerusalemu (Yeremia sura ya 52). Hata katika hukumu hii kali zaidi, Mungu anaahidi kuirejesha Yuda katika nchi ambayo Mungu alikuwa amewapa (Yeremia 29:10).

Ishara: Yeremia 23: 5-6 inatoa unabii wa Masihi anayekuja, Yesu Kristo. Nabii anaeleza juu yake kuwa Yeye ni kama Tawi kutoka nyumba ya Daudi (Mst 5;. Mathayo 1), Mfalme ambaye atatawala katika hekima na haki (Mst 5, Ufunuo 11:15.). Ni Kristo ambaye hatimaye atatambuliwa na Israeli kama Masihi wake wa kweli kama anavyotoa wokovu kwa wateule wake (Mst 6;. Warumi 11:26).

Vitendo Tekelezi: Nabii Yeremia alikuwa na ujumbe mgumu zaidi kuwasilisha. Yeremia alipenda Yuda, lakini alimpenda Mungu zaidi. Chungu Kama ilivyokuwa chungu kwa Yeremia kutoa ujumbe thabiti wa hukumu kwa watu wake mwenyewe, Yeremia alikuwa mtiifu kwa kile Mungu alimwambia kufanya na kusema. Yeremia alitumai na kuomba kwa ajili ya huruma kutoka kwa Mungu kwa ajili ya Yuda, lakini pia aliamini kuwa Mungu alikuwa mwema, mwenye haki, na mwadilifu. Sisi pia lazima tumtii Mungu, hata wakati ni vigumu, tutambue mapenzi ya Mungu kuwa muhimu zaidi kuliko mahitaji yetu wenyewe, na kuamini kwamba Mungu, katika hekima yake isiyo na kipimo na mpango wake kamilifu, ataleta mabora zaidi kwa watoto wake (Warumi 8:28) .

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Yeremia
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries