settings icon
share icon

Kitabu cha Yakobo

Mwandishi: Mwandishi wa hii nyaraka (barua) ni Yakobo, pia aitwaye Yakobo mwadilifu, ambaye anadaiwa kuwa ndugu wa Yesu Kristo (Mathayo 13:55; Marko 6: 3). Yakobo hakuwa muumini (Yohana 7: 3-5) mpaka baada ya ufufuo (Matendo 1:14; 1 Wakorintho 15: 7; Wagalatia 1:19). Yeye akawa mkuu wa kanisa la Yerusalemu na anatajwa kwanza kama nguzo ya kanisa (Wagalatia 2: 9).

Tarehe ya kuandikwa: Kitabu cha Yakobo pengine ndicho kitabu kongwe zaidi cha Agano Jipya, kilichoandikwa labda mapema kama 45 BK, kabla ya baraza la kwanza la Yerusalemu mnamo 50 BK. Yakobo aliuawa mnamo mwaka 62 BK, kwa mujibu wa mwanahistoria Yusufu.

Kusudi la Kuandika: Baadhi wanadhani kwamba waraka huu uliandikwa kwa mjibu wa tafsiri yenye raghba ya mafundisho ya Paulo kuhusu imani. Mtazamo huu uliokithiri, uitwao upinga-sheria, ulishikilia kwamba kupitia kwa imani katika Kristo mtu ni huru kabisa kutoka kwa sheria zote za Agano la Kale, ushikiliaji mno wa sheria, sheria zote za kidunia, na maadili yote ya jamii. Kitabu cha Yakobo kimeelekezwa kwa Wakristo Wayahudi waliotawanyika miongoni mwa mataifa yote (Yakobo 1: 1). Martin Luther, ambaye alichukia sana barua hii na kuiita "barua ya kubuniwa," alishindwa kutambua kwamba mafundisho ya Yakobo kuhusu kazi yalikamilisha - si kupinga - mafundisho ya Paulo juu ya imani. Wakati mafundisho ya kipaulo yaliangazia sana kwa kuhesabiwa haki kwetu na Mungu, mafundisho ya Yakobo yanaangazia sana kazi ambazo zinaruhusu huko kuhesabiwa haki. Yakobo alikuwa anaandika kwa Wayahudi kuwatia moyo kuendelea kukua katika imani hii mpya ya Kikristo. Yakobo anasisitiza kwamba matendo mazuri kiasili yatatokea kutoka kwa wale ambao wamejazwa na Roho na anauliza iwapo mtu anaweza kuwa na imani au kukosa imani ya kuokoa ikiwa matunda ya roho hayawezi kuonekana, kiasi kama Paulo anaeleza katika Wagalatia 5: 22-23.

Mistari muhimu: Yakobo 1: 2-3: "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi."

Yakobo 1:19: "Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi, Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, si mwepesi wa kusema; wala kukasirika."

Yakobo 2: 17-18: “Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu. "

Yakobo 3: 5: "Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana."

Yakobo 5: 16b: "Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."

Muhtasari kwa kifupi: kitabu cha Yakobo kinaonyesha kutembea kwa imani kupitia kwa dini ya kweli (1: 1-27), imani ya kweli (2: 1-3: 12) na hekima ya kweli (3: 13-5: 20). Kitabu hiki kina umuhimu sawa sambamba na Mahubiri ya Yesu ya Mlimani katika Mathayo 5-7. Yakobo ananza katika sura ya kwanza kwa kueleza sifa za jumla za kutembea kwa imani. Katika sura pili na mwanzo wa sura ya tatu anajadili haki za kijamii na mahubiri juu ya imani katika matendo. Kisha analinganisha na kupinga tofauti kati ya hekima ya kidunia na hekima ya kimungu na anatuuliza kugeuka kutoka kwa mabaya na kumkaribia Mungu. Yakobo anatoa kukemea kukali maalumu kwa matajiri ambao huweka akiba na wale ambao wanajitegemea. Hatimaye anamalizia kwa kuwatia moyo waumini kuwa wavumilivu katika mateso, wakiomba na kujaliana na kuegemeza imani yetu kwa ushirika.

Mashirikisho: Kitabu cha Yakobo ni maelezo ya mwisho ya uhusiano kati ya imani na matendo. Hivyo ndivyo walivyokolea katika Sheria za Musa na mfumo wake wa kazi Wakristo Wayahudi ambao Yakobo aliwaandikia kwamba alitumia muda mwingi kuelezea ukweli mgumu kwamba hakuna mtu atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria (Wagalatia 2:16). Anawatangazia kwamba hata kama wajaribu kadri ya uwezo wao kushika sheria mbalimbali zote na kanuni, kufanya hivyo haiwezekani, na kuvunja sehemu kidogo sana ya sheria kuliwafanya wenye hatia ya yote (Yakobo 2:10) kwa sababu sheria ni kitu kimoja na kuvunja sehemu moja yake ni kuivunja yote.

Vitendo Tekelezi: Tunaona katika kitabu cha Yakobo changamoto kwa wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo siyo tu "waseme kusema," bali "watembee kusema" Wakati kutembea kwa imani kwetu, kuwa na uhakika, kunahitaji ukuaji wa ufahamu kuhusu Neno, Yakobo anatusihi tusiachie hapo. Wakristo wengi watapata waraka huu kuwa na changamoto kwa vile Yakobo anatoa majukumu 60 katika mistari 108 tu. Yeye analenga katika ukweli wa maneno ya Yesu katika mafundisho Mlimani na kutupea motisha kutenda kulingana na kile alifundisha.

Waraka pia unapuuzilia mbali dhana kwamba mtu anaweza kuwa Mkristo na bado kuendelea kuishi katika dhambi, bila kuonyesha matunda ya haki. "Imani," kama hiyo Yakobo anasema, ina ushirika na mapepo ambao "wanaamini na kutetemeka" (Yakobo 2:19). Hata hivyo "imani" kama hiyo haiwezi kuokoa kwa sababu haithibitishwi kwa matendo ambayo uambatana na imani ya kweli ya kuokoa (Waefeso 2:10). Matendo mema si chanzo cha wokovu, bali ni matokeo yake.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Yakobo
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries