settings icon
share icon

Kitabu cha Warumi

Mwandishi: Warumi 1: 1 inatambua mwandishi wa kitabu cha Warumi kama mtume Paulo. Warumi 16:22 inaonyesha kwamba Paulo alitumia mtu mmoja jina Tertio kunakili maneno yake.

Tarehe ya kuandikwa: kitabu cha Warumi huenda kiliandikwa 56-58 BK.

Kusudi la Kuandika: Kama nyaraka zote za Paulo kwa makanisa, kusudi lake la kuandika lilikuwa kutangaza utukufu wa Bwana Yesu Kristo kwa kufundisha kanuni za mafundisho na kuadilisha na kuwatia moyo waumini ambao wangepokea barua yake. Wale ambao Paulo alijali sana ni wale ambao barua hii iliandikiwa-wale walio katika Roma ambao a " walipendwa na Mungu na walioitwa kuwa watakatifu" (Warumi 1: 7). Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ni raia wa Roma, alikuwa na mapenzi ya kipekee kwa wale waliokuwa katika mkutano wa waumini katika Roma. Tangu hadi hapa hakuwa ametembelea kanisa katika Rumi, barua hii pia ilitumika kama utangulizi wake kwao.

Mistari muhimu: Warumi 1:16, "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uwezo wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."

Warumi 3: 9-11, "Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi; Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja; hakuna afahamuye; hakuna amtafutaye Mungu. "

Warumi 3:21, "Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii."

Warumi 3:23: "Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu."

Warumi 5: 8, "Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi."

Warumi 6:23 "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."

Warumi 8: 9, "Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. "

Warumi 8:28: "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake."

Warumi 8: 37-39, "Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika,wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wente uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu. "

Warumi 10: 9-10, "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. "

Warumi 12: 1, "Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana."

Warumi 12:19, "Wapenzi, msijilipie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana, "

Warumi 16:17, "Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. "

Muhtasari kwa kifupi: Paulo alikuwa na msisimko juu ya kuwa na uwezo wa kuhudumu mwishowe katika kanisa hili, na kila mtu alikuwa anafahamu vizuri ukweli huo(Warumi 1: 8-15). Barua kwa Waroma iliandikwa kutoka Korintho tu kabla ya safari ya Paulo kwenda Yerusalemu kutoa sadaka zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya maskini huko. Alikuwa na lengo la kwenda Roma na kisha kwenye Hispania (Warumi 15:24), lakini mipango yake ilikatizwa wakati alikamatwa katika Yerusalemu. Hatimaye angeweza kwenda Roma kama mfungwa. Fibi, ambaye alikuwa mshirika wa kanisa la Kenkrea karibu na Korintho (Warumi 16: 1), huenda ndiye alipeleka barua Roma.

kitabu cha Warumi kimsingi ni kazi ya mafundisho na kinaweza kugawanywa katika sehemu nne: haki inayohitajika, 1: 18-3: 20; haki inayotolewa, 3: 21-8: 39; haki inayoonyeshwa, 9: 1-11: 36; haki inayotekelezwa, 12: 1-15: 13. Dhamira kuu ya barua hii ni dhahiri bila shaka-haki. Kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, Paulo kwanza analaani watu wote kwa dhambi zao. Anaonyesha matakwa yake ya kuhubiri ukweli wa Neno la Mungu kwa wale walio katika Roma. Ilikuwa tumaini lake kuwa na uhakika walikuwa wanakaa kwenye njia ya haki. Yeye kwa nguvu anasema kuwa haiionei haya Injili (Warumi 1:16), kwa sababu ni nguvu ambayo kila mtu anaokolewa kwayo.

kitabu cha Warumi kinatueleza kumhusu Mungu, yeye ni nani na amefanya nini. Kinatuambia kuhusu Yesu Kristo, nini kifo chake kilitimiza. Kinatuambia kuhusu sisi wenyewe, nini tulikuwa bila Kristo na sisi ni nani baada ya kuamini katika Kristo. Paulo anasema kwamba Mungu hakudai watu warekebishwe maisha yao kabla ya kuja kwa Kristo. Wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu.

Mashirikisho: Paulo anatumia watu kadhaa wa Agano la Kale na matukio kama mifano ya ukweli wa utukufu katika kitabu cha Warumi. Ibrahimu aliamini na haki ilihesabiwa kwake kwa imani yake, na si kwa matendo yake (Warumi 4: 1-5). Katika Warumi 4: 6-9, Paulo anarejelea kwa Daudi ambaye alirudia ukweli huo: "Heri waliosamehewa makosa yao, na waliositiriwa dhambi zao. Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi. "Paulo anatumia Adamu kuelezea Warumi mafundisho ya dhambi tulizorithi na anatumia hadithi ya Sarai na Isaka, mwana wa ahadi, ili kuonyesha kanuni za Wakristo kuwa wana wa ahadi ya neema kuu ya Mungu kupitia kwa Kristo. Katika sura 9-11, Paulo anakumbuka historia ya taifa la Israeli na kutangaza kwamba Mungu hatimaye hajakataa kabisa Israeli (Warumi 11: 11-12), lakini amewaruhusu kuwa na "mashaka" tu mpaka idadi kamili ya watu wa mataifa mengine wapate wokovu.

Vitendo Tekelezi: kitabu cha Warumi kinaweka wazi kwamba hakuna kitu tunaweza kufanya ili kujiokoa wenyewe. Kila tendo "zuri" tumewahi fanya ni kama tambara chafu mbele ya Mungu. Hivyo ndivyo tulivyo wafu katika makosa na dhambi zetu ambapo kwamba ni tu neema na huruma ya Mungu inaweza kutuokoa. Mungu alionyesha neema hiyo na huruma kwa kumtuma Mwana wake, Yesu Kristo, ili afe msalabani kwa ajili yetu. Tunapogeuza maisha yetu kwa Kristo, hatudhibitiwa tena na asili yetu ya dhambi, ila tunadhibitiwa na Roho. Ikiwa tutakiri kwamba Yesu ni Bwana, na kuamini kwamba Yeye alifufuliwa kutoka kwa wafu, tumeokoka, na kuzaliwa upya. Tunahitaji kuishi maisha yetu yaliyotolewa kwa Mungu kama sadaka iliyo hai kwake. Ibada ya Mungu ambaye alituokoa inapaswa kuwa hitaji letu la juu. Labda utendaji bora wa Warumi unaweza ukawa kutekeleza Warumi 1:16 na kutoiionea haya Injili. Badala yake, hebu wote tuwe waaminifu katika kuitangaza!

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kitabu cha Warumi
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries